Kutoka Mtandaoni: Staa mkongwe wa Bongo Movies, Jacob Stephen ‘JB’
amempongeza staa mwenzake Salma Jabu ‘Nisha’ kwa jitihada zake za
kuzitangaza kazi zake zaidi kupitia ukursa wake kwenye mtandao picha wa
Instagram ambapo hadi leo anawatu zaidi ya laki moja na nusu wanao
mfuatilia.
Napenda kuongea kutokana moyoni kwamba navutiwa na jinsi dada huyu
anavyo jitahidi.hongera.kila nikipitia acc yako mara nyingi unaongelea
juu ya kazi zako.hongera. endelea kupambana,”JB aliandika hayo mara
baada ya kuweka picha hiyo hapo juu akiwa na Nisha.
Hakika Nisha anastahili pongezi kwa matumizi hayo mazuri ya mtandao picha wa Instagram, mastaa wengine wajifunze kutoka kwake.
Mzee wa Ubuyu