Staa mkongwe wa filamu za vichekesho King Majuto ameamua kufanya filamu zake mwenyewe na si zakushirikishwa kama kipindi cha nyuma.
Akizungumza na gazeti la Nipasge wiki hii, Majuto alisema ameamua kuwa anatoa filamu zake baada ya kuona vijana wadogo ambao wameanza kazi za uigizaji hivi karibuni wanafanya kazi za kutengeneza filamu zao wenyewe katika kampuni zao.
Majuto alisema anatafakari mbinu za kujiekea mazingira mazuri kwa ajili ya kutengeneza filamu zake.
“Nimechoka kucheza katika filamu za watu” alisema Majuto ambaye anaongoza kwa kucheza filamu nyingi kwa sasa.