Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini,Sulemani Nyambui akizungumzia namna
mbio hizo zitakavyokuwa ikiwa ni pamoja na njia zitakazokuwa zikitumika
kwa washiriki wa mbio ndefu.Kulia ni Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon
2014,Innocent Melleck na kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa
Dar es Salaam,Tullo Chambo.
Mratibu
wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck (katikati) akikabidhi
ada ya Sh. Milioni mbili kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Raidha Tanzania
(RT),Suleiman Nyambui (kulia) huku Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa
Dar es Salaam,Tullo Chambo akizungumza machache akishuhudia.
Mratibu
wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck akikabidhi ada ya Sh.
Milioni moja kwa Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo
Chambo
Mratibu
wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck akionyesha moja ya fomu
za kujiunga na mbio hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam leo juu ya maandalizi ya mbio hizo
kwa mwaka huu ambazo zinataji kufanyika Desemba 7,2014,huku Mgeni rasmi
akitazamiwa kuwa ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete huku Zaidi ya wanariadha
elfu kumi na tano kukadiriwa kushiriki kwa mara ya kwanza.kushoto ni
Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo
Mratibu
wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck (katikati) akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam leo juu ya
maandalizi ya mbio hizo kwa mwaka huu ambapo zinataji kufanyika Desemba
7,2014.Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini,Sulemani
Nyambui na kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es
Salaam,Tullo Chambo
ZAIDI
ya wanariadha 15,000 kutoka ndani na nje wanatarajiwa kuthibitisha
kushiriki katika mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika
Desemba 7 kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa mbio hizo, Innocent Melleck,
alisema kuwa maandalizi yako katika hatua za mwisho huku akimtaja Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa
kuongoa mbio hizo.
Melleck
pia alikabidhi ada ya Sh. Milioni mbili kwa Chama cha Raidha Tanzania
(RT) na Sh. Milioni moja kwa wenyeji Chama cha Raidha Mkoa wa Dar es
Salaam (DAAA), ili kupata kibali cha kuendesha mbio hizo.
Mratibu
huyo alisema kuwa fomu kwa ajili ya kushiriki mbio hizo zimeanza
kutolewa jana na jijini zinapatikana katika maduka yote ya TSN, huku pia
zikitolewa kwenye mikoa ya Arusha, Moshi mkoani Kilimanjaro na Leaders.
“Tunawashukuru
wadau wote walioshiriki katika kujiandaa kushiriki mbio hizo hasa klabu
za jogging ambazo zinahamasisha wanariadha kushiriki mbio hizo zenye
kuhamasisha Amani, ushirikiano na mshikamano,” alisema Melleck.
Katibu
Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, alisema kuwa chama kimeialika mikoa yote
ya Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Afrika Mashariki na mataifa
mengine ambayo yako tayari kushiriki mbio hizo zitakazofanyika sambamba
na sherehe za Uhuru wa Tanzania.
Nyambui
alisema kuwa wanariadha wamejiandaa kuonyesha vipaji vyao na wanaamini
yataendelea kukuza vipaji vyao kulitangaza jina la Tanzania.
Naye Mjumbe wa DAAA, Tullo Chambo, alisema kwamba chama kimeshiriki
kuanzia hatua ya awali na wanawahakikishia wadau kuwa mbio za mwaka huu
zitakuwa na mafanikio.
Chambo alisema kuwa wanazipongeza klabu na makundi yote yanayoendelea
kujiandaa kushiriki mbio hizo na kila kitu kitafanyika kwa kufuata
taratibu za kiufundi.
Melleck
alitoa rai kwa makampuni na mashirika pia watu binafsi kujitokeza kwa
wingi ili kuweza kudhamini mbio hizi kwani bado nafasi ipo kwa wale wote
wenye nia ya kudhamini kwa mwaka huu.
Mbio
za Uhurumarathon kwa mwaka huu zinadhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini
TBL kupitia kinywaji chake Grandmalt,Maji ya Uhui,Azam Tv,Tbc
1,Mwananchi Communications Ltd,Magazeti ya Uhuru,Jambo Leo,Michuzi
media,CxC Africa,Kitwe General Traders,Samsung,Cokacola,Tindwa Mediacal
Service,Gazeti la TABIBU,Konyagi,na TSN SUPERMARKETS.




