Nov 12, 2014

AJALI MBAYA: Watu Kadhaa Wapoteza Maisha leo Asubuhi baada ya basi kupinduka Kahama


Watu kadhaa wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa asubuhi hii kwenye ajali ya basi la Wibonela lililokuwa likitoka Kahama kwenda Dar lililopinduka eneo la kona ya Phantom, Kahama.
 
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliopelekea dereva wa basi kushindwa kulimudu lilipofika kwenye kona ya Phantom na kupelekea kuingia mtaroni na kupinduka.
 
Idadi kamili ya waliopoteza maisha na majeruhi kwenye ajali hiyo bado haijafahamika.
 

Baadhi ya miili tayari imetolewa katika eneo la ajali huku majeruhi nao wakikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya Kahama kwa matibabu.

Katika  hatua  nyingine, mtu  mmoja  amechomwa  moto  na  wananchi  wenye  hasira  kali  baada  ya  kunaswa  akiwaibia  Majeruhi  badala  ya  kutoa  msaada.