Nov 12, 2013

VIJANA MKOANI KILIMANJARO WAHIMIZWA UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MILENIA


 Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungmza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro juu ya umuhimu wa kujihusisha na kazi za Umoja wa Mataifa wakati wa ziara za kutembelea shule mbalimbali za mkoa huo.

Na Ripota  wetu.
Vijana wa shule za sekondari nchini wameaswa kuwa mabalozi wazuri pindi watakapomaliza masomo yao juu ya kuhamasisha utekelezaji wa malengo ya milenia kwa sababu ni dira ya maendelo ya taifa na dunia kwa ujumla.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Wasichana Kibosho, Lyamungo na Umbwe sekondari hivi karibuni, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema malengo ya milenia yanagusa Nyanja zote za maendelo kwa vijana walio na wasio mashuleni.

Bi. Nkhoma amewataka wanafunzi wafanye kazi za kujitolea na kuhakikisha wanapeleka elimu waliopata kupitia vilabu vya Umoja wa Mataifa kwa jamii na kuhamasisha dhana ya kujitolea kwa maslahi ya nchi.
“kila ndani ya saa moja tuna vijana 50 ambao wanapata maambukizi ya VVU kati ya miaka 14-24 ambao wengi kati ya hao ni Wasichana, hivyo msijihusishe na masuala ya mapenzi mnapokuwa mashuleni”, amesema Bi. Nkhoma.






Bi. Usia Nkhoma Ledama akionyesha takwimu za Mimba za Utotoni zilizotolewa hivi karibuni (“Young People Today. Time to Act Now”) ambapo asilimia 25 ya watoto wa kike chini ya miaka 14 wanapata wakiwa mashuleni.

source jiachie blog