Kutoka
kushoto ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dkt. Philip Mpango,
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile, Kamishna wa
Sera Bw. Beda Shallanda na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya
wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa majadiliano ya mkutano wa madola.
WATANZANIA WAHUDHURIA MKUTANO WA JUMUIYA
YA MADOLA
Wakati mikutano mingine ikiendelea hapa
mjini Washington DC, Tanzania pia inashiriki katika mkutano wa Jumuiya ya
Madola ambao utafanyika kwa siku mbili mfululizo. Mkutano huu unahudhuriwa na
wajumbe wote ambao ni nchi wanachama.
Katika mkutano huo kikubwa
kilichojadiliwa ni kuhusiana na suala zima la biashara, ni namna gani biashara
inaweza kufanyika na kwamba nchi zetu haziko vizuri sana katika uwanja huu wa
kimataifa. Katika mkutano huo walijadili ni jinsi gani wanaweza kufanikisha lengo
la kuanzisha mfuko ambao utatumika kusaidia biashara ‘trade facilitation’.
Katika majadiliano yaliyokuwa
yakifanyika wajumbe wengi walipenda kujua kwamba ni tofauti gani
mfuko huo mpya utaleta ili nchi zetu ziweze kunufaika. Hiki ni kitu
kikubwa zaidi kilicho wagusa wajumbe wengi.
Akizungumza na vyombo vya habari Dkt.
Silvacius Likwelile ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye alisema
kuwa”katika mkutano huu jambo ambalo limezungumziwa sana ni kuhusu
kuondoa vikwazo ambavyo mara nyingi tunawekewa ili kufikia masoko katika
ulimwengu”. Aliendelea kusema kuwa, ni imani yetu kwamba tume ya madola
itafanyia kazi masuala hayo ili hatimaye tuwe na msimamo mmoja wa kuweza
kusaidia ukuaji wa biashara katika nchi zetu. Mkutano huu utaendelea tena kesho
na inategemewa utakuwa na mafanikio makubwa.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji MkuuWizara ya Fedha
Washington D.C
08/10/2013
picha na jiachie+wamburababu




