Oct 14, 2013

MCHUNGAJI WA KANISA ANGLIKANA GONGO LA MBOTO AFUMWA LIVE AKIVUNJA AMRI YA 6 GEST NA MKE WA TU GESTI BILA WOGA


TOFAUTI na inavyoaminika na wengi kuwa watumishi wa Mungu ni watu safi,
safari hii Mchungaji Obed Ntimba wa Kanisa la Anglikana Gongo la Mboto,
Dar es Salaam amejikuta akivunja agano la Muumba baada ya kunaswa gesti
akiwa na mke wa mtu.

Tukio hilo la aibu lilimkuta mchungaji huyo Ijumaa iliyopita saa saba na
nusu za mchana katika gesti moja (jina lipo) iliyopo nyuma ya Jengo la
Ubungo Plaza jijini Dar.

Siku moja kabla ya tukio, makachero wetu walitonywa kuhusu dhambi hiyo
na mtu wa karibu na watu hao akisema kuwa anaumia kwa sababu mchungaji
huyo ana mke na watoto na mwanamke huyo, Rose ni mke wa mwanajeshi kwa
hiyo aliamini tendo wanalotaka kulifanya ni uovu katika jamii.

Mtoa habari wetu huyo alisema tukio hilo lilipangwa kukamilika kesho
yake Ijumaa katika gesti hiyo ndipo kazi ya kuwafuatilia hatua moja
baada ya nyingine ilianza.
 
Ijumaa saa sita mchana, mtonyaji wetu alipiga simu  na kuweka wazi
kwamba wawili hao wapo njiani kuelekea gesti, kila mmoja kwa usafiri wake.

Ndipo makachero wetu  walipowatonya polisi na kuambatana nao mpaka
kwenye gesti hiyo na kujipanga kwa mbinu za kisasa za kutoonwa na ‘adui’.

Makachero hao  walifanikiwa kupata ramani ya chumba walichoingia wawili
hao ambapo ‘rumu’ namba 1B ndiyo iliwasilishwa kwamba Rose na mchungaji
wake wamo humo.

Saa saba na nusu mchana, Makachero wetu na polisi waliingia hadi
mapokezi ya gesti hiyo kwa kificho na kutoa maelekezo kwa mhudumu.
Mhudumu aliongozana nao hadi mlangoni na kugonga lakini haukufunguliwa.

*BAADA YA DAKIKA TANO*
Wakati mlango huo ukigongwa na mhudumu bila kufunguliwa, mchungaji huyo
alisikika akisema na kuuliza:
“Subirini kwanza.”
“Lakini ninyi ni akina nani?”

Baada ya dakika tano kupita, mlango ulifunguliwa, mchungaji akakutana na
macho ya timu nzima. Alipigwa butwaa asijue la kufanya huku akitetemeka,
Rose alikuwa ndani ya khanga moja!

*MCHUNGAJI MSOBEMSOBE HADI POLISI*
Polisi waliwabeba msobemsobe wote hadi Kituo cha Polisi cha
Urafiki-Ubungo, Dar ambapo kila mmoja alianza kujieleza.

*MCHUNGAJI APANGULIA HUDUMA YA KIROHO*
Kituoni hapo, Mchungaji Ntimba alipobanwa kuhusu sababu za kuingia gesti
na mke wa mtu, alisema waliingia kwa ajili ya huduma ya kiroho kwani
mwanamke huyo alikuwa anataka kufungua kanisa ndipo alipomuomba yeye
amsaidie.

“Mimi sikuwa na lengo baya jamani. Huyu dada alihitaji kufungua kanisa,
akaniambia ili nimshauri hawezi kukaa  sehemu ya wazi kwa kuwa mume wake
ni mwanajeshi anaweza kuonekana na watu wakampa taarifa.

“Ndipo nikaamua kwenda naye katika nyumba ile ya kulala wageni kwani
wageni wengi wanaokuja kwa ajili ya huduma, wakitokea nchi mbalimbali
huwa wanalala pale na wahusika wa pale wananifahamu sana.

*“Baada ya kuingia gesti nilibanwa na haja ndogo, nikaenda kujisaidia.
Cha kushangaza niliporudi nilimkuta huyu dada amevua nguo zote na kuanza
kunishawishi lakini sikuwa na lengo hilo jamani,”* alijitetea mchungaji
huyo.

Baadhi ya picha zilizopo  zinamuonesha mchungaji huyo akiwa amevaa
suruali lakini amesahau kufunga zipu huku kondom zikiwa pembeni kitandani!

***MSIKIE MKE WA MTU SASA*
Baada ya mchungaji kutoa maelezo yake, mke wa mtu naye alianza
kutiririka ya kwake huku akionesha ushahidi wa meseji za simu ambazo
mchungaji huyo alikuwa akimtumia akimshawishi kumpa penzi.

*“Huyu mchungaji nilikwenda kwake kwa lengo la kufanya kazi kanisani
lakini kuanzia hapo amekuwa akinishawishi kuwa anataka nimpe penzi ili
aweze kuniweka katika sehemu nzuri kanisani.*

“Nilikuwa nakataa, lakini akasema tukutane pale gesti tuongee zaidi.
Nilikataa kukutana gesti, akaniambia pale ni ofisini, mara nyingi akiwa
anaongea na waumini mambo muhimu ya huduma ya kiroho huwa anakutana nao
pale.

*“Nikakubali lakini kabla hata hatujaongea chochote alianza kuvua nguo
zake na kuanza kunilazimisha tufanye mapenzi huku akiwa na ‘kinga’
kabisa na mimi nikavua nguo lakini kabla hajatimiza lengo lake ndipo
wakaingia watu wakiwa na askari.*

“Mimi nashukuru sana kwa sababu hawa ndiyo wameniokoa. Nilikuwa
nikisikia habari za huyu mchungaji kuwa ana tabia ya kuwafanyia
wasichana wengi vitendo hivyo na kweli leo ndiyo nimeamini,” alieleza
mwanamke huyo.

Katibu wa kanisa hilo (jina halikupatikana mara moja) alimuombea msamaha
mchungaji kwa waandishi huku akionesha kuumizwa na kitendo hicho baada
ya kuoneshwa ushahidi na kukiri kwamba una ukweli tofauti na alivyokuwa
akifikiria awali kabla ya kuachiwa kwa dhamana.