Oct 13, 2013

HALMASHAURI YA IRINGA YAPONGEZWA KWA MIRADI BORA KATIKA MBIO ZA MWENGE


Mbunge  wa viti maalum  mkoa wa Iringa  Ritta Kabati (kushoto ) na Lediana  Mafulu  wakishiriki  kucheza ngoma na kikundi cha hamasa  Iringa  vijijini leo 
 

 Kiongozi wa kitaifa wa  mbio za mwenge Bw  Juma Alli Simai  akimtwika ndoo ya maji mkazi wa kijiji Lyamgungwe Bi Renata Msemba mara  baada ya  kuzindua mradi  huo wa maji leo











Kiongozi  wa mbio  za mwenge  Kitaifa Juma Alli Simai  ameipongeza Halmaashauri ya  wilaya ya Iringa kwa usimamizi mzuri wa miradi 11  ya kimaendeleo na kutaka  wilaya nyingine  kuiga mfano huo.

Miradi  hiyo imejengwa kwa kiasi cha zaidi ya Tsh bilioni 1.7  imepongezwa baada ya mbio za mwenge wa Uhuru 2013  kuitembelea na kuizindua rasmi leo.