Oct 8, 2013

EXCLUSIVE : MZEE MAJUTO ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA 2015, SOMA HAPA ALICHOKISEMA MZEE MAJUTO



king majuto


MCHEKESHAJI mkongwe nchini, Amri Athuman 'King Majuto' ametangaza nia
yake ya kujitosa kwenye siasa akitaka kuwania Ubunge katika Jimbo la
Tanga Mjini katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
Akihojiwa na kituo cha Clouds FM, Mzee Majuto mwenye umri zaidi ya miaka 60, alisema Mungu
akimjalia atajitosa kwenye ubunge jimboni humo kupitia
Chama cha Mapinduzi (CCM), akidai kiu hiyo imechochewa na mafanikio yawasanii waliojitosa kwenye siasa na kufanya vyema.
Mzee Majuto alisema, uzoefu alionao katika kuishi kwake mjini Tangaitamwezesha kuwatatulia kero na kuwaletea maendeleo ya kweli wananchiwenzake iwapo Mungu atamjalia katika kusudio lake.
Kadhalika Muigizaji, ambaye pia ni mtayarishaji na muongozaji wa filamunchini, Yekonia Watson 'Amani' amesema matarajio yake miaka michache ijayo ni kujitosa kwenye siasa akitaka kuwania Ubunge kabla ya kuangalianafasi ya juu zaidi kwa maana Rais.
Akizungumza na MICHARAZO jioni hii, Watson alisema anaamini ana uwezo nakipawa cha uongozi hivyo anaweka mambo sawa kabla ya kujitosa jumla kwenye duru hilo, japo yeye hakuweka bayana atajitosa kupitia chama gani.
"Kwa sasa ni mapema mno, ila nitaanzia Ubunge kisha kuangalia nafasi ya juu, ila muhimu Mungu anipe uhai na umri wa kufanikisha hilo," alisema mkali huyo anayejiandaa kuachia filamu yake mpya iitwayo 'Uwanja wa Vita' aliyoigiza na wasanii kadhaa nyota akiwamo Irene Uwoya.