Mwantanga Ame
MTOTO wa miezi 10, aliyetambuliwa kwa jina la Fahazal mkazi wa Kivunge
amefikishwa mbele ya serikali ya mkoa wa kaskazini Unguja, baada ya mama
yake mzazi kusema amekuwa akitokewa na maajabu na kwamba jamii iombe dua
ili kunusuru kutokea vifo.
Mtoto huyo, ambaye anaishi katika kijiji cha Changani Kivunge wilaya ya
Kaskazini ‘A’ Unguja, ameonesha maajabu, baada ya kuanza kusema akiwa na
umri wa miezi miwili, kwa kutaja majina ya Mwenyezi Mungu, Mtume
Muhammad (SAW) na maneno ya kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Mkuu wa wilaya hiyo, Riziki Juma Simai, akizungumza na Zanzibar Leo,
amethibitisha kuwepo mtoto huyo.
Alisema mtoto huyo amefikishwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na familia yake
baada ya mama yake aliyefahamika kwa jina moja la Dawa, kutakiwa
kuwasilisha ujumbe alionao mtoto huyo kwa jamii.
Alisema kabla ya kuzaliwa, mama yake alisema kuwa alikutwa na mambo ya
maajabu baada ya kujiwa na kiumbe akimueleza uwezo wa mtoto wake wakati
akiwa tumboni na kumchagulia jina la kumpa baada ya kuzaliwa.
Mkuu wa wilaya huyo alisema, kiumbe hicho kilichokuwa katika mazingira
yasioelezeka pia kilimtabiria mama huyo kwamba atazaa mtoto wa kiume.
Pia alimuambia baada ya mtoto huyo kuzaliwa atakuwa na mambo ya ajabu na
kumtaka kumtunza na asimuogope na baadae kiumbe hicho kiliondoka.
Alisema baada ya tukio hilo, na siku zake za kuzaa kutimia alijifungua
mtoto wa kiume na kumpa jina la Fahazal na ndipo alipoanza kushuhudua
maajabu ikiwa ni pamoja na kuzungumza akiwa na miezi miwili.
Alisema mtoto huyo alikuwa akitamka maneno ya kumtukuza Mwenyezi Mungu
ikiwemo Allwah, Yaraabi na kutaja jina la Mtume (SAW) huku akiwataja kwa
majina watu waliokuwemo nyumbani kwao.
Mkuu wa wilaya hiyo alisema hivi sasa mtoto huyo, amekuwa akiwasomea dua
watu wanaofikishwa kwake kwa matatizo ambapo huonesha ishara ya kuinua
mikono juu ya kuitikia dua wakati ikisomwa.
Alisema kwa muda mrefu, familia yake iliendelea kuishi naye, lakini mama
yake alifuatwa tena na kiumbe hicho na kumtaka kufikisha ujumbe wa mtoto
huyo mbele ya jamii akitaka jamii iombe dua kwa wingi kwani vifo vingi
vinaweza kutokea nchini.
Alisema kiumbe hcho kilirudi baada ya mama wa mtoto huyo kupuuza ujumbe
wa mwanzo aliopewa na ndipo alipoamua kutafuta watu wa kumsaidia ambapo
walimuelekeza kufuata viongozi wa dini.
Alisema, baada mama huyo kupokea ujumbe huo, aliamua kuutekeleza kwa
kuwafuata baadhi ya walimu katika kijiji hicho kuelezea mkasa huo, ili
aweze kupata msaada.
Viongozi wa dini walimtaka mama huyo, kulifikisha suala hilo katika
ngazi ya serikali, kutokana uzito wake kwa jamii, ambapo walimshauri
kuonana na uongozi wa mkoa.
Mkuu huyo wa wilaya alisema, jana asubuhi, alimpokea mama huyo akiwa na
mtoto wake pamoja na shahidi ambaye ni mkaazi wa kijiji hicho ambapo
walithibitisha maajabu ya mtoto huyo.
Alisema mtoto huyo huzungumza baadhi ya wakati na kwamba anazungumza
lugha tofauti ikiwemo kiingereza, kiarabu.
Alisema wameifikisha familia hiyo kwa Mkuu wa Mkoa ili kufanyiwa
mahojiano zaidi ambapo serikali itajua nini la kufanya hapo baadae.
Alisema wanalazimika kulifanyia kazi suala hilo, kwa vile tayari
imetolewa tahadhari ya kutokea balaa litakalowahusisha watu wengi.

habari kwa hisani ya bongoclan+babuwambura