Maboresho ya Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, Toleo la Mwaka 2024 yameweka msingi mpya wa kulinda mila, desturi na utamaduni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 Bungeni jijini Dodoma Mei 28, 2025.
Amesema Sera hiyo imejumuisha masuala mapya ya kimkakati ikiwemo kutumia Kiswahili kama nyenzo ya diplomasia, uchumi wa buluu, kuimarisha ushiriki wa Diaspora katika maendeleo ya Taifa, usimamizi wa Mikataba na Itifaki za Kimataifa, mazingira na mabadiliko ya tabianchi na usawa wa jinsia na vijana.
.jpeg)


.jpeg)