Mgombea wa Republican, Trump ameshinda
urai wa Marekani ambapo mpaka sasa naongoza kwa kura 279, Clinton kura
218 za wajumbe kati ya kura 538.
Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani,
Mshindi alitakiwa kushinda angalau majimbo 270 lakin Bw. Trump amevuka
lengo na kufikisha kura 279 mpaka sasa.

Trump ashinda jimbo la Pennsylvania
Mgombea wa Republican Donald Trump
ameshinda jimbo la Pennsylvania kwa asilimia 49 dhidi ya 48 za Clinton.
Jimbo hilo lina kura 20 za wajumbe. Clinton sasa ana jumla ya kura 245
za wajumbe na Trump 218. Bwana Trump anahitaji kura 26 tu ili aweze
kufikisha kura 270 ambazo atahesabiwa kuwa mshindi.
Clinton kushinda Virginia
ABC News wamekadiria kwamba Hillary Clinton ndiye mshindi jimbo la
Virginia, moja ya majimbo yaliyokuwa yanashindaniwa. Jimbo hilo lina
kura 13 za wajumbe.
Trump ndiye mshindi Ohio
ABC News wamekadiria kwamba Donald Trump atashinda jimbo muhimu la Ohio. Jimbo hilo lina kura 18 za wajumbe.
Trump ashinda jimbo la Montana
Mgombea wa Republican Donald Trump
ameshinda jimbo la Montana. Jimbo hilo lina kura 3 za wajumbe. Clinton
sasa ana jumla ya kura 104 za wajumbe na Trump 140.
Trump ‘ana nafasi nzuri’ – New York Times
Gazeti la New York Times, ambalo
limekuwa likiunga mkono Hillary Clinton, linasema mfumo wake wa kompyuta
kwa sasa unabashiri uwezekano wa Trump kushinda kuwa 53%.
Louisiana kwenda kwa Trump
ABC News wanakadiria kwamba Donald Trump atashinda jimbo la Louisiana.
Jimbo hilo limepigia kura mgombea wa
Republican katika chaguzi nne mtawalia lakini waliunga mkono Bill
Clinton mwaka 1992 na 1996.
Jimbo hilo huwa halichukuliwi kama ngome ya Republican kama yalivyo majimbo mengine jirani.Jimbo hilo lina kura nane za wajumbe.
Clinton ashinda jimbo la Washington
Hillary Clinton ameshinda jimbo la
Washington kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Jimbo hilo lina kura 12
za wajumbe. Sasa Trump ana kura 222 za wajumbe na Clinton 209 za
wajumbe. Mshindi anahitaji kura 270.
Trump ndiye mshindi Florida
ABC News wametangaza kwamba makadirio
yao yanaonyesha Trump ameshinda jimbo muhimu la Florida.Sasa Trump ana
kura 222 za wajumbe na Clinton 197 za wajumbe. Mshindi anahitaji kura
270.
Jimbo hilo huwa muhimu sana kwa mgombea yeyote.
Jimbo hilo lilimpigia Obama mwaka 2008
na 2012 (Democratic), lakini George W Bush (Republican) alishinda
uchaguzi uliotangulia 2000 na 2004. Jambo la kushangaza ni kuwa alikuwa
mbele na kura 537 pekee mwaka 2000.
Hata hivyo, ilichukua siku 36 kwake
kuthibitishwa kuwa mshindi, kwa hivyo iwapo wagombea watakaribiana sana
usitarajie matokeo yatangazwe haraka.
Clinton mshindi Connecticut, kwa mujibu wa ABC
Hillary Clinton ameshinda jimbo la
Connecticut, ngome ya chama cha Democratic ambapo amejishindia kura saba
za wajumbe, kwa mujibu wa ABC News. Clinton sasa ana kura za wajumbe
104 na Trump 129.
Trump mshindi jimbo la Arkansas
Trump anakadiriwa kushinda jimbo la Arkansas kwa mujibu wa ABC News. Jimbo hilo lina kura sita za wajumbe.
Kwa kura za wajumbe, sasa Trump ana 129 na Clinton 97