
Wajumbe
wa Bodi ya wakurugenzi wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje, wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Leo
Jijini Dar es Salaam.

aziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiongea na
wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)
wakati akiizindua leo Jijini Dar es Salaam, ambapo ameitaka bodi hiyo
kushika miradi mikubwa ya uwekezaji na kuhakikisha inairudisha katika
hali yake ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia uanzishwaji
na uendelezaji wa viwanda.

Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje(kulia)
akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa
Maendeleo (NDC) Dkt. Samweli Nyantahe nyaraka mbalimbali
zitakazomuongoza katika utendaji kazi.

Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiwa katika
picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Taifa la
Maendeleo (NDC) mara baada ya kuizindua leo Jijini Dar Es Salaam.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.