
Fundi wa TANESCO, akiwa kazini leo Septemba 3, 2016.

Meneja
Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO),
ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme,
Injinia Theodory Bayona.(katikati), akisimamia kazi hiyo leo Septemba 3,
2016.

Kaimu
Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Leila Muhaji,
akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la mradi
NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
WAHANDISI,
na mafundi wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), kwa
kushirikia na wale wa kampuni za Kijapani za Yachiyo Engineering Co
Limited, Takaoka na National Construction Co. Limited, wameanza kazi ya
uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupooza na
kusambaza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam, imeanza leo Septemba 3,
2016.
Kazi
kubwa inayofanyika hivi sasa ni kubadilisha laini kutoka umeme mdogo
kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili
kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora ulio
juu.
“Ikumbukwe
kwamba, hapa tulikuwa na laini mbili (waya mbili) zilizokuwa na uwezo
wa kusafirisha umeme kiasi cha Megawati 120 kila moja, kutoka hapa
Ubungo kwenda kituo cha Ilala, lakini kazi inayofanyika sasa, ni
kubadili njia hizo (waya za umeme), ambazo zitakuwa na uwezo wa
kupitisha kiasi cha umeme wenye Megawati 220 kila moja,” Alifafanua
Meneja Muandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, ambaye pia ndiye
Meneja wa wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory
Bayona.
Kwa mantiki hiyo, kazi inayofanyika leo hii itawezesha umeme
utakaokuwa ukisafirishwa kutoka hapa Ubungo kwenda Ilala, kuwa na jumla
ya Megawati 440 kwa laini zote mbili, tofauti na hapo awali ambapo uwezo
wa kusafirisha umeme ulikuwa Megawati 240 tu,” Alisema.
Kazi ikikamilika wakazi wa jiji la Dar es Salaam, watakuwa wakipata umeme wa uhakika, na ulio bora, alifafanua Injinia Bayona.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania,
(TANESCO), Leila Muhaji, amewaomba wananchi kuwa wavumilivu katika
kipindi hiki ambapo Shirika linafanya juhudi kubwa za kuwapatia umeme wa
uhakika wananchi kwa kuimarisha miundombinu yake,.
“Ili kuwawezesha mafundi wetu kufanya kazi katika mazingira
salama, tutakuwa tukikata umeme kuanzia leo hii Septemba 3 na umeme
utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa
utaratibu na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11,
Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016.” Alifafanua Leila, na kuwaomba
wananc hi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki.
Mradi huu ulioanza Februari 2015 na unaotarajiwa kukamilika Juni
2017 unatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Japan (JICA) .

Tsutomu Sato, wa kampuni ya Takaoka ya Japan, akiwa kazini

Mafundi wa TANESCO, wakitayarisha nyaya hizo mpya

Fundi wa TANESCO, akifunga kikombe wakati wa kazi ya kubadilisha
miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye kituo kikuu cha kupooza na
kusambaza umeme cha Ubungo, jijini Dar es Salaam

Raphael Mjata, Msimamizi Mkuu wa Njia Kuu za Umeme, akionyesha uwezo wa kituo cha Ubungo cha kupooza umeme wenye kilovolti 132.

Mafundi wa TANESCO na kampuni ya National Construction Company Limited, wakivuta nyaya hizo mpya

Hizi ndio nyaya zitakazofungwa kwenye laini mbili za kusafirisha umeme kutoka kituo cha kupooza na kusafirisha umeme cha Ubungo.


Mhandisi Bayona, akielezea waandishi wa habari mwenendo wa kazi hiyo

Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Leila Muhaji, na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Henry Kilasila, wakiwa kazini.


Mhandisi Bayona (kulia), akijadiliana jambo na Wahandisi wenzake,
Yasutaka Osawa, (kushoto), ambaye ni mwakilishi katika mradi wa
kuboresha umeme jiji la Dar es Salaam, kutoka kampuni ya Takaoka
Engineering Co Ltd, na Mhandisi Ahmed Mmingwa, ambaye ni Msimamizi wa
Mradi kutoka TANESCO.

Mwakilishi wa kampuni ya Kijapani ya Yachiyo Engineering Co.
Limited, Tamai Masayuki,akizungumza na waandishi wa habari kuhsuu
maendeleo ya uboreshaji huo

Wahandisi wakijadiliana jambo

Fundi wa TANESCO akiwa kazini.

Kazi inaendelea

Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme
Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha
miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.(katikati), Kaimu Meneja
Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kulia) na Afisa Habari wa Shirika
hilo makao makuu, Henry Kilasila, (wakwanza kushoto) na waandishi wa
habari, wakitembelea eneo la mradi mapema leo asubuhi Septemba 3, 2016
ambapo kazi ilianza kwa kasi

Wafanyakazi wa TANESCO chumba cha ufuatiliaji mwenendo wa umeme (control room) wakiwa akzini.

Chumba cha kufutialia mwenendo wa umeme jijini Dar es Salaam, (Control room), cha TANESCO-Ubungo sub station)