
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia
Ackson akiongoza sala wakati wa ufunguzi wa kikao cha Bunge leo Mjini
Dodoma.

Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)
Mhe. Selemani Jafo akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo alisema
serikali ipo katika uhakiki wa maombi ya maeneo mapya utawala kwa
kuangalia vigezo katika kuanzisha maeneo hayo.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Prof. Joyce
Ndalichako akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo alisema serikali
serikali itaendelea kuongeza udahili wa walimu wa sayansi katika vyuo
vya elimu ili kuweza kukidhi mahitaji husika.


Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akijibu wakati wa
kikao cha bunge ambapo aliwaeleza wabunge kuwa Katiba ya Nchi ibara ya
3(2) inaeleza kuwa mambo yote yanayohusu uandikishaji na uendeshaji wa
vyama vya siasa nchini yatasimamiswa kwa mujibu wa masharti ya katiba na
sheria iliyotungwa ba Bunge

Waziri
Wizara ya Mmabo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu wakati wa
kikao cha bunge ambapo alisisitiza watanzania kufuata sheria za nchi na
iwapo utakiuka jeshi la polisi litachukuwa hatua bila kujali itikadi ya
chama chochote cha siasa.

Mbunge
wa Jimbo la Tarime Vijini Mhe. John Heche akichangia hoja kuhusu
tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati wa kikao cha Bunge leo Mjini
Dodoma.

Mbunge
wa Jimbo la Muleba Kusini Mhe. Prof. Anna Tibaijuka akichangia hoja
kuhusu tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati wa kikao cha Bunge leo
Mjini Dodoma ambapo mbali na mambo mengine wabunge wamekubaliana
kuchangia posho ya siku moja kwa ajili ya wahanga wa tetemeko mkoani
Kagera.

Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakisimama kwa dakika moja
kuungana na wahanga wa tetemeko lililotokea mkoani Kagera.

Waziri
Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.
George Simbachawene akitoa taarifa ya serikali kuhusu tetemeko la ardhi
lililotokea hivi karibuni Mkoani Kagera. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO