
Aliyekuwa
muwezeshaji katika Mkutano huo Profesa Aldo Lupala Mhadhiri kutoka Chuo
Kikuu Ardhi ambaye ni Mkuu wa Kitivo cha Usanifu Majengo akitoa
mwongozo wakati wa mkutano huo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania, Dr. Stephen Nindi akizungumza jambo juu ya Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa pamoja kuhakikisha maeneo yanapimwa na kuweka mpango mzuri wa Matumizi Bora ya Ardhi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania, Dr. Stephen Nindi akizungumza jambo juu ya Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa pamoja kuhakikisha maeneo yanapimwa na kuweka mpango mzuri wa Matumizi Bora ya Ardhi.

Wadau wa mkutano huo wakiendelea kufuatiliamkutano huo

Mratibu
wa Mradi wa Ardhi yetu kutoka CARE International Tanzania Mary Ndaro
akifafanua jambo wakati wa mkutano huo wa kikosi kazi

Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo akielezea mikakati mbalimbali waliyonayo kuhusu mpango wa matumizi bora ya ardhi

Bw.
Amos Mfuga kutoka Tume ya Taifa Mipango na Matumizi ya Ardhi akichangia
jambo ikiwa ni pamoja na Tume kuweka vipaumbele kama kuangalia na
kumaliza migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini


Wadau wa mkutano huo wa kikosi kazi kutoka Sehemu mbalimbali wakiendelea na mkutano huo

Bw. Mdubi kutoka CARE International Tanzania akichangia jambo wakati wa Mkutano huo wa kikosi kazi

Naomi Shadrack kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Tanzania akielezea namna shirika hilo likifanya kazi hapa Nchini na jinsi wanavyoshiriki katika mpango huo wa matumizi bora ya Ardhi

Bw. Jamboi kutoka Ujamaa Community akielezea ushiriki wao katika mpango wa matumizi bora ya ardhi

Bw.Emanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii akichangia jambo juu ya ushiriki wao katika kikosi kazi hicho.

John Lugaso mmoja wa viongozi kutoka Chama cha wafugaji Tanzania , akieleza malengo ya chama hicho ikiwa ni pamoja na mipango ya baadae ya uanzishaji wa viwanda mbalimbali kwa ajili ya bidhaa zinazotokana na mifugo.

Mkutano ukiendelea
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa
Katika
kupanga matumizi bora ya ardhi nchini Tanzania ikiwa na lengo la jamii
kutumia rasilimali hiyo vizuri kwa matumizi ya kawaida, Serikali imesema
kuwa hadi sasa imefikia takribani vijiji 1645 na Wilaya 40 nchi nzima.
Kutokana na ufinyu wa bajeti na kasi ndogo ya upimaji bado kuna vijiji
11,393 ambavyo havijafikiwa.
Akizungumza
Mkoani Morogoro ,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya
Ardhi,Dkt Stephen Nindi wakati wa Mkutano wa Kikosi kazi cha kuanda
mpango kazi wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa maendeleo ya Ardhi
nchini.
Pia
Mkutano huo ulijadili kuhusu migogoro ya ardhi inayoendelea nchini na
mipango ya matumizi ya ardhi kama inaweza kusaidia kupunguza migogoro
hiyo,uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka Serikalini ,taasisi na
Mashirika mbalimbali yanayosimamia masuala ya ardhi.
Alisema
serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanashirikiana kwa pamoja
kuhakikisha maeneo yanapimwa na kuweka mpango mzuri wa matumizi ya
ardhi kwa matumizi yaliyokusudiwa katika kujadiliana ni namna gani
wataona njia zinazofaa kutumika kukamilisha zoezi hilo la upimaji kwa
vijiji vingine ikiwemo kuwepo kwa teknolojia mpya ya upimaji na kuwepo
kwa bajeti ya kutosha.
Aliongeza
kuwa lengo la kupima,kumilikisha na Kupanga kila kipande cha ardhi ni
pamoja na kuhakikisha ardhi inakuwa na matumizi mazuri katika nchi.
Dkt.Nindi
alisema tayari serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wametoa
elimu katika timu za wilaya 100 kuwawezesha kujua
kupima,kupanga,kumilikisha ,kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi
ya ardhi .
Kwa
upande wake Mratibu wa Programu ya Mradi ya Ardhi yetu kutoka Shirika
la Kimataifa la CARE nchini Tanzania ,Mary Ndaro alisema mpaka sasa ni
miaka mingi tangu nchi ipate uhuru kasi ya upimaji wa maeneo imekua
ndogo .
Alisema
kama nchi inajiandaa kuwa na wawekezaji wengi zaidi inatakiwa
kuhakikisha inakuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi ambayo baadae
haitaweza kuleta mgogoro wowote kati ya wanakijiji na muwekezaji.Aliongeza
kuwa kwa sasa kati ya vijiji 12,545 nchi nzima ni vijiji 1645 ndiyo
tayari vina mipango ya matumizi ya ardhi mpaka sasa.
Vijiji vingi bado havina mipango kutokana na ufinyu wa bajeti na kuwepo kwa kasi ndogo ya upangaji.Ndaro alisema lengo la mkutano huo wa wadau ni kuona ni namna gani vijiji vilivyobaki kati ya vijiji 12,545 vinapangiwa matumizi ya ardhi, kunakuwa na ushirikiano wa karibu wa wadau na namna vipi wanashirikiana kutatua migogoro ya ardhi ambayo inazidi kuongezeka.
Vijiji vingi bado havina mipango kutokana na ufinyu wa bajeti na kuwepo kwa kasi ndogo ya upangaji.Ndaro alisema lengo la mkutano huo wa wadau ni kuona ni namna gani vijiji vilivyobaki kati ya vijiji 12,545 vinapangiwa matumizi ya ardhi, kunakuwa na ushirikiano wa karibu wa wadau na namna vipi wanashirikiana kutatua migogoro ya ardhi ambayo inazidi kuongezeka.
“Pamoja
na kuwepo kwa kasi ndogo ya upangaji matumizi ya ardhi, bado kuna
changamoto ya kutoheshimu mipango ya matumizi ya ardhi
iliyokwishaandaliwa ambapo utakuta kijiji tayari kimepangwa lakini
kinakuja kukatwa katikati na kuwa vijiji viwili au zaidi,”alisema
Alisema
serikali inapaswa kuweka mipango ya matumizi ya ardhi ipasavyo ili
kuweza kudhibiti hali ya migogoro ya ardhi kati ya watumiaji mbalimbali,
mfano baina ya wawekezaji na wanavijiji kwa kupanga matumizi ya
ardhi.“Serikali inapoita wawekezaji nchini inapaswa pia kuhakikisha
mpango ya matumizi bora ya ardhi inayoeleweka kwa lengo la manufaa ya
mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,”alisema