Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesema kuwa Tanzania
imeweza kupunguza zaidi ya tani 216 sawa na asilimia 86 ya kiasi cha matumizi
ya kemikali haribifu chini ya programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya
kemikali hizo.
Waziri Makamba
ameyasema hayo leo mjini Dodoma kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Hifadhi
ya Tabaka la Ozoni Septemba 16, mwaka huu.
Waziri Makamba
amesema kuwa upungufu huo umetokana na jitihada za utekelezaji wa mpango wa
usimamizi wa vipozi uliowezesha uwekaji wa mtambo wa kunasa na kurejeleza
kemikali uliopo katika kituo cha Tanzania cha uzalishaji bora na teknolojia
endelevu.
Aidha, Waziri Makamba
alisema kuwa mpango huo uliwezesha ununuzi na usambazaji wa mashine 20 za
kunasa na 5 za kunasa na kurejeleza gesi katika karakana 20 na vituo vitano vya
kanda vya kunasa na kusafisha gesi chakavu za majokofu na viyoyozi katika vyuo
vya VETA vya Mwanza, Dar es Salaam, Kigoma, Mbeya na Mkokotoni Zanzibar.
Mbali na hayo, Waziri
Makamba ametoa wito kwa wananchi kushiriki katika kupunguza na kuondosha
madhara ya Tabaka la Ozoni yanayosababishwa na bidhaa zinazotumika majumbani au
sehemu za biashara.
Waiziri Makamba amesema
kuwa ili kuhifadhi tabaka la Ozoni nchini, jamii kwa ujumla inapaswa kuepuka
kuingiza gesi zilizopigwa marufuku nchini sambamba na vifaa vinavyotumia gesi
haribifu ikiwemo majokofu na viyoyozi vilivyokwishatumika na ambavyo vinatumia
vipoozi aina ya R11 NA R12.
Aidha, wananchi
wametakiwa kuepika kutupa ovyo majokofu ya zamani ama vifaa vya kuzima moto
vyenye kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni aina ya CFCs na halon na
kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa mafundi ama mamlaka husika.