Sep 16, 2016

Taarifa kutoka TCU: Kigezo kipya cha ufaulu kinachohitajika kupata nafasi katika Vyuo mbalimbali

tcu-3

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), sasa imefanya mabadiliko katika kigezo kinachohitajika kwa watu wanastahili kuendelea na masomo ya Chuo, tangu kutangazwa kwa sifa mpya Julai 11 mwaka huu. Taarifa mpya imetolewa na tume hiyo ikitaja kigezo kipya cha ufaulu kwa waombaji wenye sifa ya stashahada (Diploma), ambapo kigezo kimeshushwa kutoka GPA ya 3.5 hadi GPA ya 3.0, ili kutoa nafasi kwa waombaji wengi zaidi kupata nafasi katika vyuo mbalimbali.
Taarifa hiyo pia imeshusha kigezo kwa waombaji wenye Full Technician Certificate (FTC) kutoka wastani wa B hadi kufikia wastani wa C.
Aidha TCU imewatangazia watu wote wenye  uhitaji wa kuendelea na vyuo vikuu wenye GPA ya 3.0 kwa Stashahada na wastani wa C kwa wenye FTC watume maombi kupitia TCU kabla ya Septemba 23, mwaka huu.
Pia TCU imesema kuwa wale ambao walikuwa tayari wamekwishatuma maombi, na wanakidhi vigezo hivi hawatakiwi kuomba tena.

tcu-1 tcu-2