Sep 2, 2016

Rais Magufuli Awasili Pemba kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Mbili

3.Dkt. Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika Kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma na wameshiriki Dua ya kumuombea Marehemu iliyoongozwa na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kiislamu na Kikristo.
jpm4Akizungumza mara baada Dua, Rais Magufuli amesema anamkumbuka Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa ukarimu wake, upendo, kutojikweza, kutobagua watu na kudumisha amani katika siku zote za maisha yake.
Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kudumisha kwa vitendo amani aliyoisimamia Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.
jpm6

“Mimi najua huko aliko Marehemu Dkt. Omar Ali Juma anaendelea kuliombea Taifa hili ili hiyo amani aliyoihubiri katika maisha yake, ili huo upendo aliousimamia katika maisha yake, ili huo uchapa kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote tuweze kuendeleza kwa mioyo yetu yote” Amesema Rais Magufuli.
jpm7 
Rais Magufuli akiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma Makamu wa Rais wa zamani katika awamu ya Tatu katika kijiji cha Wawi Bigilini katika Wilaya ya Chake chake Pemba.
jpm3Mama Janeth Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma Makamu wa Rais wa zamani kijiji cha Wawi Bigilini kisiwani katika Wilaya ya Chake chake Pemba.

Rais Magufuli akitazama kikundi cha ngoma baada ya kutua Pemba ambapo pia ameenda kuzulu kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Omary Ali Juma. Baadaye saa tisa alasiri atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale, Pemba. Picha na Ikulu