Sep 2, 2016

Aliyanena Rais Magufuli Leo Akiwa Pemba

magufuli (2)  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Pemba katika Uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba.
magufuli na shein (1)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuhutubia mkutano katika Uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba.
magufuli na shein (2)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Pemba katika Uwanja wa Gombani ya Kale, Chake Chake, kisiwani Pemba.
PICHA NA IKULU

Aliyanena Rais Magufuli leo akiwa Pemba
“Dokta Shein una support yangu yote, ukiona umemshindwa mtu, nambie mimi uone kama itapita hata dk 5”
“Wakati tukinadi kwenye kampeni mimi na Shein, tulisema tunataka Tanzania yenye viwanda”
“Hawezi mtu kuja kujenga kiwanda kama kuna vurugu, watu hawasalimiani, hamna amani.”
“Vijana wa Pemba hawana ajira kama walivyo vijana wa bara, kwa hiyo vijana lazima tuwe wa mbele kujenga amani.”
“Na mimi nataka nikwambie Dk. Shein, wewe ndiyo Rais, na naona umekuwa mpole sana,
“Upole uweke pembeni, uwe mkali kidogo, usikubali kuchezewa na mtu,
“Libya ilikuwa nchi ya amani, wakatumiwa watu wachache kwa ahadi za uongo, sasa Libya hakukaliki, watu wanakimbia…”
“Libya watu wanamwaga damu kila siku, kwa sababu watu walichezea amani.”
Mna bahati ndugu zangu, mna rais mpole sana , hata sura yake nzuri tu, Lakini pia ametoka Pemba, mnataka nini!? Mnataka malaika aje aongoze!