Kasisi Nicholas Chamberlain, amesema
kuwa walioshiriki katika mchakato wa kumteua mwaka uliopita walialewa
fika mwelekeo wake wa jinsia.
”Watu wanajua nashiriki mapenzi ya
jinsia moja, lakini si kitu cha kwanza nachoweza kumwambia yeyote.
Jinsia ni sehemu ya yule niliye, lakini ni kazi yangu ya kitume ambayo
ninataka kuiangazia .”
Watu wanajua nashiriki mapenzi ya jinsia
moja, lakini si kitu cha kwanza nachoweza kumwambia yeyote. Jinsia ni
sehemu ya yule niliye mimi, lakini ni kazi yangu ya kitume ambayo
ninataka kuiangaziaNicholas Chamberlain, Asakofu
Nicholas Chamberlain anasema hata hivyo anafuata kanuni za kanisa zinazosema kuwa haruhusiwi kuoa.
Msemaji wa kanisa la England amesema:
“Nicholas hajamkera yeyote na amekua wazi na mkweli ukiuliza. Suala lake
si la siri, ingawa ni la kibinafsi kama ilivyo kwa wale walio katika
mahusiano ya kimapenzi .”
Inadhaniwa kuwa hakuna askofu yeyote anayehudumu aliyewahi kutangaza hadharani msimamo wake wa kingono.
Kanisa la kianglikana kote duniani
limegawanyika sana miaka ya hivi karibuni kuhusu masuala yanayohusu
mwelekeo wa kijinsia na kutawazwa kwa makasisi walio katika mapenzi ya
jinsia moja.