Fujo
zimezuka katika Mji Mkuu wa Gabon, Libreville baada ya Rais Ali Bongo
kutangazwa jana Jumatano mchana kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais
uliofanyika Jumamosi iliyopita, Agosti 27, 2016, kwa kupata asilimia
49.8% ya kura, akifuatwa na mpinzani wake Bw Ping aliyepata asilimia
48.2 % ya kura, huku wa kitofautiana kura 5,594 pekee.
Jean Ping
Mgombea wa upinzani kwenye uchaguzi huo,
Jean Ping ambaye pia ni shemeji wa rais Ali Bongo amesema watu wawili
wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya vikosi vya usalama kuvamia
makao makuu ya chama chake.
Serikali imesema inawaandama “wahalifu wenye silaha” ambao awali walikuwa wameteketeza majengo ya bunge.
Bw
Ping amepinga matokeo ya urais ambayo yalionyesha Rais Bongo alishinda
uchaguzi kwa kura chache. Hii inampa fursa ya kuongoza taifa hilo kwa
muhula mwingine wa miaka saba.
“Walishambulia
mwendo wa saa 01:00 (00:00 GMT). Ni kikosi cha wanajeshi walinzi wa
rais. Walikuwa wanarusha mabomu kutoka kwa helikopta na kisha baadaye
wakashambulia kutoka ardhini,” Bw Ping, ambaye hakuwa katika makao makuu
hayo wakati huo, alisema awali.
Rais Ali Bongo
Ping ameomba usaidizi kutoka kwa jamii
ya kimataifa kulinda raia huku akieleza kuwa uchaguzi huo ulijaa
udanganyifu na “hakuna ajuaye” hasa nani alishinda.
Waandamanaji
waliingia barabarani muda mfupi baada ya tangazo kutolewa na kuchoma
moto majengo ya bunge na kukabiliana na polisi wa kuzima fujo.
Upande
wa Bw Ping unasema takwimu kutoka ngome za rais huyo zinaonesha
asilimia 99 ya wapiga kura walijitokeza. Ameomba takwimu za wapiga kura
kutoka kila kituo zitolewe wazi.
Marekani
na Umoja wa Ulaya wametoa wito kura hizo ziwekwe wazi huku katibu mkuu
wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon naye akihimiza utulivu.
Bw Bongo aliingia madarakani mwaka 2009, baada ya kifo cha babake aliyechukua madaraka 1967.
Kabla ya kuingia kwenye siasa, Bw Ping alikuwa mwanadiplomasia ambaye alihudumu kama mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika