Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda amewatangazia walimu wa mkoa huo, kuanza kusafiri bure
kwenye treni baada ya kuingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania
(TRL).
Hatua hiyo imekuja ikiwa miezi michache
imepita tangu, kiongozi huyo kuanzisha mfumo wa walimu kusafiri bure
kwenye daladala wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Makonda alisema walimu watasaifiri bure katika njia za Stesheni-Ubungo
Maziwa na Stesheni –Pugu ambako treni zinafanya safari zake.
“Kinachotakiwa ni kuwa na vitambulisho
kutoka kwa wakuu wa shule, wakionyesha hakuna atakayewahoji hivyo
watasafiri bure,”alisema Makonda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa alisema walimu watasafirishwa kwa nidhamu kubwa.
chanzo bofya hapa