Kesi hiyo inayomkabili aliyekuwa
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (pichani kati) Harry
Kitilya na wenzake dhidi ya mashtaka manane ikiwamo la kutakatisha fedha
na walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Aprili Mosi Mwaka huu.
Akisoma uamuzi huo Jaji Edson
Mkasimongwa alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili mahakama
yake imeona Hakimu Mchauru wa Mahakama ya Kisutu alikosea kuliondoa
shtaka hilo na kwamba shtaka la kutakatisha fedha litabaki kama
lilivyofunguliwa katika hati ya mashtaka.
“mahakama ya Kisutu ilikosea kisheria
kulifuta shtaka la 8 na ninaamuru kurejesha kumbukumbuku ya jalada la
kesi hii kwa ajili ya kuendelea kusikilozwa” alisema Jaji Mkasimongwa.
Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni
Miss Tanzania 1996 Shose Sinare na Sioi Solomon ambao walisomewa
mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mchauru.
Awali, jopo la mawakili wa utetezi
liliwasilisha maombi ya kuliondoa shtaka la nane ya kutakatisha fedha na
mahaka?a ya Kisutu ilikubali na kuliondoa.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Osward Tibabyekomya ulowasilisha nia ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dar es
Salaam alitupilia mbali rufaa hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande
zote mbili kwamba mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza rufaa ya
kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha.
Upande wa Jamhuri ulikata rufani katika Mahakama ya Rufani Tanzania.
Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jopo
la Majaji watatu ikiongozwa na Bernad Luanda,Salum Masati na Aristoclas
Kaijage liliamuru jalada la kesi hiyo kurejeshwa mahakama kuu na
kupangiwa jaji mwingine wa kusikiliza rufaa ya Jamhuri.
Jalada hilo lilipangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Mkasimongwa