MREMBO ambaye jina lake liko juu
kwa sasa kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed
‘Shilole’ hivi karibuni amewaka baada ya kubanwa maswali juu ya tetesi
za uhusiano wake na Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Juma Mchopanga ‘Jay
Moe’.
Akistorisha na Uwazi Showbiz,
Shilole alifunguka kuwa hana uhusiano na mkali huyo wa ngoma ya Pesa
Madafu na hajawahi kufikiria kutoka naye na anawashangaa watu
wanaomhusisha kuwa kwenye mahaba na Jay Moe.
“Watu bwana wanashindwa kufuata yao
wanakalia kuchonga yawenzao, mimi Jay Moe ni kaka yangu, tumeshibana na
hatuna uhusiano wowote,” alisema Shilole.
Kwa upande wa Jay Moe amefunguka kupitia
kwenye mitandao ya kijamii juu ya kuzisikia tetesi za yeye kutoka
kimapenzi na Shilole, amedai pia hazina ukweli wowote maana mwanadada
huyo ni mshikaji wake wa karibu tu!