WAZIRI
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesitisha
malipo ya posho za kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini
ambao wanaofanya mafunzo kwa vitendo (practical training) ‘field’ baada
ya kubaini kuwepo na wanafunzi hewa zaidi ya 1000 vyuoni.
Prof.
Ndalichako amesema wizara yake imezuia posho hizo kwa muda wa wiki
mbili wakati wizara hiyo ikiwa inafanya uhakiki ili kuwabaini wanafunzi
hewa zaidi pamoja na wahusika kuwachukulia hatua za kisheria.
Aidha
Prof. Ndalichako amewaagiza wakuu wote wa vyuo kuwasilisha taarifa za
wanafunzi wao wizarani ili zoezi la kukagua na kubaini uahalali wa
wanafunzi hao kuwepo vyuoni na wale watakaoonekana kuwa wana sifa
watapatiwa posho zao za kujikimu mapema na kuendelea na masomo.
CHANZO: EA RADIO