Marekani
Rais Barack
Obama wa Marekani amesema kuwa iwapo mgombea urais wa Chama cha
Republican, Donald Trump atashinda katika uchaguzi ujao wa rais wa nchi
hiyo yeye ataondoka Marekani.
Barack Obama Rais wa Marekani ameliambia
Gazeti la World News Politics kwamba, kama Trump atashinda uchaguzo
ujao wa rais, yeye na familia yake wataondoka Marekani bila ya mapema.
Obama amesema kuwa amejadiliana na mke
na watoto wake kuhusu suala hilo la kukubaliana kwenda nje ya Marekani
iwapo Trump atashinda kiti cha rais wa nchi hiyo.
Inasemekana kwamba, iwapo ataondoka
Marekani, Rais Obama anakusudia kuishi nchini Canada na kwamba tayari
maudhui ya kuhama kwa Obama imejadiliwa na Waziri Mkuu wa Canada, Justin
Trudeau.
Matamshi na misimamo ya kushangaza ya
mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Republican, Donald
Trump imekabiliwa na upinzani mkali ndani na nje ya Marekani.