Audio: Lema Amjibu Waziri Mwigulu Kuhusu Maandamano Septemba 1
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba hivi karibuni akiwa
ziarani mkoani Mtwara alizungumza na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoani
humo na kusema kuwa CHADEMA wasithubutu kuandamana kwani kwa kufanya
hivyo si kuwa watakuwa wanatingisha kiberiti cha njiti, bali watakuwa
wanachezea gesi. Amesema kuwa sio kila kitu mtu anatakiwa kujaribu kwa
sababu vingine huenda vikakuumiza.