Aiagiza TANESCO kuweka Umeme ndani ya wiki mbili watumishi wahamieAwaomba wananchi kutoa ushirikiano Barabara YA Lupaso- Bujesi ikamilike
MKUU wa MKOA wa Mbeya
leo amefanya ziara ya kikazi halmashauri YA Busokelo wilaya ya Rungwe
kwa kukagua ujenzi wa nyumba 14 zilizojengwa na NHC kwa ajili ya
watumishi wa halmashauri ya Busokelo pamoja na nyumba
hizo
kukamilika lakini watumishi hao wameshindwa kuhamia kutokana na Tanesco
kutokamilisha uingizaji wa umeme na hivyo Mkuu wa MKOA amemwagiza
Meneja wa Tanesco kukamilisha uingizaji wa Umeme katika kipindi cha wiki
mbili
hizo
kukamilika lakini watumishi hao wameshindwa kuhamia kutokana na Tanesco
kutokamilisha uingizaji wa umeme na hivyo Mkuu wa MKOA amemwagiza
Meneja wa Tanesco kukamilisha uingizaji wa Umeme katika kipindi cha wiki
mbili
Aidha amelipongeza
shirika la nyumba kwa ujenzi wa nyumba Nzuri na za bei nafuu na ameutaka
uongozi wa halmashauri hiyo kuzitunza nyumba hizo

Kuhusu uingizaji wa Maji
amemwagiza idara YA Maji na Mamlaka YA Maji MKOA kupiga kambi Busokelo
na kuingiza Maji katika nyumba hizo haraka iwezekanavyo
Kuhusu ujenzi wa
Barabara ya Lupaso- Bujesi kwa kiwango cha lami amewaomba wananchi
waruhusu Barabara hiyo kilomita 10 ijengwe baada ya kuchelewa kujengwa
kutokana na wananchi kupinga wakidai fidia .

Amewahakikishia kuwa
tathmini imeshakamilika kwa ngazi ya wilaya baadaye MKOA na mthamini
Mkuu hivyo waruhusu sasa Barabara hiyo ijengwe na fidia itafuata " Ndugu
zangu Barabara hii ilikuwa ikamilike April 2015 lakini kutokana na
madai YA fidia mliwashitaki Tanroad kesi imeendeshwa kwa miezi mitano
naomba kutamka kuwa tathimini imefanyika ngazi ya wilaya jumla sh
milioni 479 zinahitajika kulipwa fidia sasa niwaombe mruhusu Barabara
ijengwe na ikamilike March 2017"

Wananchi kwa kauli moja
wameruhusu Barabara ijengwe kwani kukamilika kwa Barabara hiyo
itarahisisha usafiri na Mazao kwa ajili ya biashara
