Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akimtangaza Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO)
ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas (kushoto) anayechukuwa
nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Assah Mwambene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
Mkurugenzi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas akieleza
mikakati yake ikiwemo kuongeza mbinu za Mawasiliano kati ya serikali na
wananchi ili kuchochea maendeleo katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano.
Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokuwa akimtangaza Mkurugenzi mya
wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw.
Hassan Abbas (kushoto) anayechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Assah
Mwambene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.