MKALI wa kurap Bongo, George
Mdemu ‘G Nako’ amefunguka kuwa watu wanaosema wasanii wa kampuni
analopigia mzigo la Weusi yaani yeye, Joh Makini pamoja na Nikki wa Pili
wanazimana kwa kutoa ngoma mfululizo hawana ufahamu mzuri kuhusu
biashara ya muziki.
Akistorisha na Uwazi Showbiz,
G Nako aliendelea kufunguka kuwa wanachofanya Weusi ni kila msanii
kusimama yeye kama yeye ambapo wanapotoa ngoma kwa kufuatana ni mbinu za
kampuni kuliteka soko muda wote.
“Ngoma zetu muda wote ni kali ni vigumu
sisi kuzimana, anapotoa Joh, nikitoa mimi na Nikki jambo hilo linafanya
sokoni tuenee sisi wenyewe. Huwezi kukwepa kuisikiliza Alosto, Perfect
Combo au wimbo wa Nikki huu Sweet Mangi, kwa hiyo watu waelewe tu hizo
ni mbinu za kibiashara zilivyo kuhakikisha soko linakuwa letu,” alisema
G Nako