
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakati
wa dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame Ikulu jijini Dar
es Salaam.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na wageni
mbalimbali katika dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Dkt.
John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim Ikulu
jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa
aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan
Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa
aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Sinde
Warioba na Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya
kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame,
Kulia ni mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.

Kijana
Omar Abdalah Ramadhan akimsalimia kwa furaha Rais Dkt. John Pombe Magufuli
katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Kijana Omar Abdalah Ramadhan akimsalimia kwa furaha
mama Janeth Magufuli mara baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kuondoka kwenye
viwanja vya maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU