Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
(katikati) akikagua DAMPO mpya la kisasa la Mji wa Mtwara ambalo ni
rafiki kwa mazingira, katika ziara yake Mkoani humo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
akipata Maelezo kuhusu uchakataji wa taka unaofanywa na kiwanda cha SBS
kutoka kwa Bw. Joseph meneja uendeshaji wa kiwanda hicho.
DAMPO
la kisasa la Mjini Mtwara ambalo ni rafiki kwa mazingira lililojengwa
kwa hisani ya bank ya Dunia kwa thamni ya shilingi bilioni 8.8, mara
DAMPO hilo litakapoanza kutumika litakuwa na uwezo wa kutengeza nishati
mbadala.
Baraza
la taifa na Hifadhi ya Mzingira NEMC limepewa mwezi mmoja na Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
kupima Vumbi, Moshi na Maji yanayotoka katika kiwana cha kuchakata taka
cha SBS kilichopo katika maeneo ya Mangamba Mjini Mtwara ili kujirisha
kama vina madhara kwa maringira na viumbe hai.
Naibu
Waziri Mpina akiwa katika muendelezo wa Ziara yake ya kukagua mazingira
na kuangalia utekelezaji wa sheria ya mazingira kwa wenye viwanda
nchini amelitaka baraza hilo kufanya kazi zake kwa umakini na
kutokukubali majibu ya vipimo toka kwa mwenyekezaji bila NEMC pia
kufanya vipimo na kupatamajibu sahihi kutokana na sababu kuwa wananchi
wamekuwa wakilalamika mara kwa mara juu ya uchavuzi wa mazingira
unaofanywa na wenye viwanda unavyo hatarisha maisha yao na mazingira kwa
ujumla.
Katika
Ziara Hiyo ya Mjini Mtwara, Naibu Waziri Mpina Pia alitembelea DAMPO la
kisasa la mjini hapo lilijengwa kwa ufadhili wa Bank ya Dunia lenye
thamani ya shilingi Bilioni 8.8 na kuwapongeza wana Mtwara kwa kupata
Dampo la kisasa ambalo ni Rafiki wa Mazingira, na kuwashauri waratibu wa
mradi huo na uongozi wa mkoa wa Mtwara kuanza kutumia DAMPO hilo ambapo
taka zitakazowekwa katika DAMPO hilo la kisasa, pia zinaweza kutumika
kutengeneza nishati mbadala.
Awali,
akitoa taarifa ya Mazingira ya Mkoa wa Mtwara, katibu Tawala wa MKoa
huo Bwana Afred Luanda, alisema kuwa Mkoa unakabiliana na changamoto
mbali mbali za kimazingira ikiwa ni pamoja na uvuvi haramu wa kutumia
mabomu, ukataji miti ovyo kwa matumizi ya kuni na mkaa, vifaa vya
uondoshaji taka pamoja na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Ziara
Ya naibu Waziri Mpina Mkoani Mtwara leo ilihusisha pia kutembelea
bandari ya mtwara ili kujionea utekelezaji wa sheria ya mazingira katika
uingizwaji wa viwatilifu na kemikali hatarishi kwa mazingira
zinazoingizwa kupitia bandari hiyo.
(Picha na Evelyn Mkokoi)