Jul 5, 2016

Naibu Waziri Annastazia Wambura akabidhi Bendera ya Taifa kwa Timu ya wasichana ya VITO FC

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Annastazia James Wambura akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland Tanzania Pekka Hukka wakati wa kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya Fc Vito Malaika inayoenda kushiriki mashindano ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu. ( Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Annastazia James Wambura (wa pili kulia) akikabidhi Bendera ya Taifa kwa nahodha timu ya mpira wa miguu Fc Vito Malaika Alia Fikiri (kushoto) kwenda kushiriki mashindano ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya umri wa miaka 11 Fc Vito Malaika na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu kushoto Mwakilishi wa Sport Development Aid Bw. Chigogolo Mohamed.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM

Serikali imeazimia kujenga na kuendeleza shule za michezo zilizopo katika mikoa yote nchini kwa kipindi hiki cha Serikali awamu ya tano.

Azimio hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wakati akizungumza na timu ya mpira ya miguu ya wasichana ya Fc Vito Malaika katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup yatakayofanyika nchini Finland Julai 8 mwaka huu.

“Azima ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuendeleza michezo nchini kwa kuibua vipaji vya michezo na kuviendeleza kuanzia wakiwa shule” Alisema Mhe. Annastazia.