
WAZIRI
wa Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana kuwachukulia
hatua watendaji wote waliosimamishwa kati katika wizara ya elimu pamoja
na kuwafikisha vyombo vya dola. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu- Elimu wa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leunard Akwilapo.

Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tarish Kibenga Katikati Naibu Katibu Mkuu- Sayansi na Ubunifu, Simon Masanjila na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Anna Mhere.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WAZIRI
wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
ametangaza kiama kwa watendaji wote wa Bodi ya Mikopo waliofanya
ubadhirifu wa fedha za wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kuwapa watu
wasiohusika.
Joyce
ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi habari jijini Dar es
Salaam leo. amesema kuwa bodi ya mikopo baada ya kufanya ukaguzi maalum
katika hoja 17 ni hoja moja imepata majibu na kuzaliwa dosari zingine
ambazo kutokuwa na mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu kwa watu ambao
wanarejesha mikopo.
Amesema
kuwa kutokana na matatizo ya bodi ya mikopo ameigiza bodi kuhakikisha
wanachukua hatua kwa watendaji wote waliosimamishwa ikiwemo kuwafikisha
vyombo vya dola.
Joyce
amesema kuwa katika dosari nyingine wanafunzi zaidi 2,000 wamepewa
mikopo katika vyuo viwili lakini wanafunzi hao hawapo katika vyuo
vilivyotajwa.
Amesema
kuwa kuna wanafunzi wanalipwa sehemu mbili ya mikopo ya bodi kwa
Tanzania Bara na Zanzibar kwa wakati mmoja huku kuna wanafunzi hawapati
mikopo kabisa na watoto wa masikini.
Aidha
amesema bodi hiyo inatakiwa kufanyia kazi dosari zote pamoja na hatua
ambazo wamezichukua kwa baadhi ya watendaji ambao wamefuja fedha za
walipa kodi.
Joyce
amesema kuwa matatizo mengine ni Baraza la Usajili wa vyuo vya Elimu
na ufundi (NACTE) kufanya kazi kazi ambazo wao wenyewe hawana uwezo nazo
ikiwemo kukagua baadhi ya vyuo ambavyo vingine vinatoa digrii ya pili.
Amesema
yote wanaangalia kwa kupitia sheria na kuona jinsi ya kuboresha
utendaji kazi kwa NACTE kufanya kazi kwa uwezo unaostahili.