Mbunge wa Mbeya mjini kwa
tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi
amesimamishwa kuhudhuria na vikao 10 vya Bunge kuanzi leo kufuatia
kitendo cha kuonyesha kidole cha kati bungeni.
Joseph Mbilinyi alitenda kosa hilo
alipokuwa akitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kile alichoeleza kuwa
kuna mbunge wa CCM aliyemtusi mama yake. Hata hivyo alipohojiwa kama
anamfahamu mbunge huyo, Mbilinyi alisema kuwa hamfahamu.
Hukumu hiyo imesomwa leo na Naibu
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya
Maadili ya Bunge kueleza kuwa kamati hiyo ilijiridhisha kuwa kitendo
kilichofanywa na mbunge huyo kuwa ni kosa.
Aidha wabunge wangine waliosimamishwa
kuhudhuria vikao vya Bunge ni pamoja na Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo,
James Ole Millya Mbunge wa Simanjiro kwa makosa yanayofanana ya kusema
uongo bungeni. Wabunge hawa wamesimamishwa kuhudhuria vikao vitano
kuanzi leo.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa ameahirisha mkutano wa tatu wa Bunge lililokuwa na lengo
la kujadili na kupitisha bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2016
2017. Kufuatia kuahirishwa huko, kuanzia kesho Julai Mosi, serikali
itaanza kutekeleza miradi na mpango mingine iliyoanishwa katika bajeti
hiyo