Dar es Salaam
MBUNGE wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu (Chadema) amesomewa shitaka lake la kutoa maneno ya
uchochezi kinyume cha kifungu namba 32 cha sheria ya magazeti.
Lissu anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi
nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mnamo June 28, 2016 kwa kumuita
‘Mkuu wa Nchi ni dikteta uchwara’.
Baada ya kusomewa shtaka hilo Lissu
amekana shtaka na kuachiwa huru kwa dhamana na hatotakiwa kusafiri nje
ya nchi bila kibali cha mahakama.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Agosti 02, 2016.