Meneja wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James
Kilaba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
kuhusiana na kuzima simu feki ifikapo kesho Juni 16 mwaka huu.
Na Chalila kibuda, Globu ya Jamii.
SIMU
ziliingizwa nchini zikiwa hazina kiwango kuzimwa rasmi kesho, katika
kuhakikisha kila mtu anatumia simu kiwango kwa usalama na ulinzi wa
nchi.
Akizungumza
na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba amesema kuwa
katika uzimaji wa simu wameshatoa elimu juu ya simu hizo.
Kilaba
amesema kuwa simu ambazo watu walibadilisha (Flash) nazo zitazimwa
kutokana na kufanya hivyo ni kosa la kisheria na mtu anayefanya hivyo
kifungo chake ni miaka 10.
Amesema
hakuna kitu chochote kinachofanya simu zisiweze kuzimwa hivyo watu
wajiandae zoezi hilo na simu zitazozimwa wametakiwa kuzihifadhi katika
mazingira salama.
Aidha
amesema katika elimu wametoa hivyo kesho kutakuwa na mkutano wa wadau
mbalimbali wa makampuni ya simu, na wamiliki wa maduka ya simu pamoja na
mafundi katika kubadilishana mawazo wakati wa kuzima simu feki.
‘’Simu
feki kesho kuzimwa hatutakuwa na mabadiliko ya kuongeza muda au
vinginevyo kutokana na elimu iliyotolewa juu simu ya feki ambazo baada
soko kushindikana mjini walipeleka vijijini’’amesema Kilaba .