
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akikata Utepe kuashiria uzinduzi
wa mapokezi ya Gari la Wagonjwa kutoka Rafiki Surgical Mission.

Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akikabidhi cheti cha Shukrani kwa
Balozi Issaya Chialo, kama sehemu ya shukrani kwa kutambua mchango wa
Rafiki Surgical Mission, walio utoa kwa Mkoa huo wa Gari la Wagonjwa.

Hilo ndilo gari lililotolewa na Rafiki Surgical Mission.
(Habari na picha zote na Afisa habari wa mkoa wa Mwanza)
Na Atley Kuni RS Mwanza.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Mhe John Mongella amepokea gari la Wagonjwa kutoka
kwa Surgical Rafiki Mission kwaajili ya kuhudumia wananchi wa mkoa huo
ambalo amelikabidhi kwa uongozi wa hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekouture
na kuwataka kuitunza kwa maslahi mapana ya wananchi wa mkoa huo.
Akizungumza
kabla yakupokea gari hilo mkuu huyo wamkoa amesema, msaada walio upokea
kutoka kwa Rafiki Mission ni masaada wakupigiwa mfano kwakuwa watu
wengi wanabarikiwa vitu vingi lakini suala lakutoa misaada wameshindwa.
RC Mongella amesema kama mkoa ukipata marafiki wa aina ya Rafiki hawana budi kuwa ng’ang’ania wasiondoke kwenye himaya yao.
“
Nafahamu hata sisi tunabarikiwa sana lakini hata siku moja hakuna mtu
aliwahi kuleta hata mkasi, hivyo lazima tufahamu kutoa ni moyo na sio
utajiri. Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amesema, karibu
asilimia tisini ya matatizo ya afya yanayo ikabili jamii ya kitanzania
yamejikita katika suala la afya ya mama na mtoto ambayo kama taifa
tukifanikiwa kuwekeza katika hili, basi matatizo mengine ya afya
yataondoka yenyewe .
“
Najua suala la mama na mtoto ni tatizo mtambuka kwa taifa, hivyo
tukiwekeza zaidi katika afya ya mama na mtoto tutakuwa tumekabili
changamoto kubwa ya masuala ya afya na itawawezesha wananchi kujikita
katika shughuli za maendeleo”, alisema Mongella
Awali
akitoa salama za Rafiki Mission, Balozi Issaya Chialo, alisema wao kama
Rafiki Mission, wanatambua matatizo yanayo ikabili jamii ya kitanzania
hususan masuala ya afya, na kwamba wao kama Rafiki Surgical mission,
hawana ubaguzi katika utoaji wa misaada kwa jamii nzima ya kitanzania.
“
Mkuu wa mkoa sisi shughuli zetu zipo katika mkoa wa Mtwara tukijikita
katika zaidi katika utafutaji wa mafuta na Gesi, lakini hiyo haituzuii
sisi kupeleka misaada pembe zingine za nchi na ndio maana leo tupo
katika mkoa wako wa Mwanza” alisema Balozi Chialo na kuongeza kuwa,
wanajisikia fahari katika hilo. Chialo ameutaka uongozi wa Hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Mwanza Seko’uture kulitunza gari hilo la wagonjwa lenye
thamani ya Mil. 40, ambalo litasaidia katika kuwakimbiza wagonjwa wenye
mahitaji maaluma sehemu mbali mbali za mkoa huo na mikoa ya jirani.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Subi, amesema hivi sasa
hospitali ya mkoa huo inakabiliwa na changamoto ya chumba cha kutolea
huduma ya upasuaji kwa akina mama, ambapo mkuu wa mkoa amemtaka Mganga
huyo wa mkoa kutenga kiasi cha Mil. 5 kutoka katika makusanyo ya ndani
ya hospitali ya mkoa huo na Mkuu wa mkoa kupitia wadau wa maendeleo
atahakikisaha kiasi kingine cha fedha kinacho salia kinapatikana
kwaajili ya ukarabati wa chumba hicho ambacho kinahitaji Mil.20 ili
kiweze kufanya kazi ya upasuaji kwa akina mama.
Hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Seko’uture, imekuwa msaada kwa wagonjwa wa
mkoa huo na mikoa ya jirani kutokana na huduma zake kuwa nzuri na
madaktari mabingwa wanaopatikana katika mkoa huo.