
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea dawa kutoka kwa Msajili
wa baraza la Famansia , Elizabeth Shakalaghe ambazo walizikamata katika
operesheni safisha maduka ya dawa leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymont Mushi akipokea baadhi ya maboksi ya dawa jijini Dar es Salaam leo.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
BARAZA
la Famasia Tanzania limekabidhi dawa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda zenye thamani ya Sh. milioni 294 zilizokamatwa
katika operesheni safisha maduka ya dawa iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi dawa hizo Msajili wa baraza hilo, Elizabeth
Shakalaghe amesema operesheni hiyo iliyofanyika katika Mikoa tisa na
walifanikiwa kukamata dawa zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 336
na kati ya dawa hizo dawa zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 11
hazifai kwa matumizi ya binadamu.Alisema dawa hizo zitasambazwa katika
hospitali zote za mkoa wa Dar es Salaam na zimehakikiwa.
Amesema
katika Mkoa wa Dar es Salaam majalada 10 yamefunguliwa mahakamani kwa
wale waliokamatwa na dawa za serikali ambayo kwa sasa yapo katika
hatua za upelelezi.
"Bado
kumekuwa na ongezeko la maduka ya dawa ambayo yanaanzishwa kinyume na
sheria na taratibu hususani katika Mkoa huu na tumebaini kwamba maduka
yaliyofugwa wakati wa operesheni yanafunguliwa wakati wa usiku na
kuendelea kutoa huduma za dawa .amesema.
Elizabeth
amesema lengo la operesheni hiyo lilikuwa ni kuwabaini na kuwachukulia
hatua stahiki wale wote watakaobainika kuvunja sheria ya famasi katika
uendeshaji na utoaji wa huduma za dawa nchini.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa dawa hizo, Mkuu wa Mkoa huu,Paul Makonda alisema
wamiliki wa maduka ya dawa ambao hawana vibali wanatakiwa kufunga maduka
hayo mara moja au kuzirudisha walikonunua huku wengine wakifanya
huduma nyingine ambayo ni tofauti na leseni walizoomba.
Makonda
amevitaka vyombo vya dola na watendaji wa ngazi ya mkoa , manispaa,
kata na mitaa kuhakikisha wanayafunga na kuyaondoa maduka yote ambayo
hayana vibali na yanayoendeshwa kinyume na sheria ya famansi nchini.
Aidha
amevitaka vyombo vya dola kufanya operesheni nyakati za usiku ili
kuweza kuwabaini na kuwachukulia hatua stahiki kwa wale watakaokaidi
maagizo ya awali na kufanya biashara wakati wa usiku kwa kizingizio
serikali imelala wakati huo.