Dar es Salaam: Mwigizaji wa
kitambo kunako Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’ ameweka wazi
kuwa, ni bora ajihusishe na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ‘kapuku’
(asiye tajiri wala maarufu) kuliko kutoa penzi lake kwa staa yeyote wa
Kibongo kwa sababu wengi wao ni ‘michosho’.
Johari (pichani) aliliambia Amani hivi
karibuni kwamba, kwa upande wake, hivi sasa kutoka na msanii au mtu
maarufu ni kujidhalilisha na kujivua nguo kwa sababu anajua tabia za
mastaa wengi wa Kibongo kuwa hawana mapenzi ya kweli na zaidi sana ni
pasua kichwa.
“Katika maisha yangu nimejifunza mambo
mengi sana ikiwemo kuumizwa hivyo kwa sasa nahitaji pumziko la moyo na
siyo karaha ya wanaume wasiokuwa waaminifu kama walivyo wanaume wengi
mastaa.
“Unajua mastaa wengi wanaume wanajijua
ni watu wenye uwezo wa kuwa na yeyote hivyo hutumia nafasi huyo kuliza
wapenzi wao jambo ambalo kwa mimi nasema nilishalitambua na sihitaji
kulia jamanis. ”
Johari aliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano
wa kimapenzi na mwigizaji ambaye ni mkurugenzi mwenzake kwenye kampuni
yao ya RJ Production, Vincent Kigosi ‘Ray’ lakini katika mazungumzo yake
hakufunguka kama anamzungumzia jamaa huyo ambaye kwa sasa moyo wake
umetua kwa ‘ndege mnana’ mwingine wa Bongo Movies, Chuchu Hans.
Lakini mbali na Johari, mastaa wengi wa
kike wamekuwa wakilalamikia kulizwa katika uhusiano na mastaa wa kiume
kuliko wao wanaume kulizwa na wanawake mastaa.
Aidha, ndoa nyingi za mastaa kwa mastaa
zimekuwa hazifiki mbali na kuvunjika kuliko ndoa za mastaa na wenza wao
wakiwa ni watu wa kawaida.
Mpaka sasa, staa mwingine ambaye analia
ndoa yake kuvunjika kwa kuolewa na staa ni Salome Urassa ‘Thea’ ambaye
ndoa yake na staa nwenzake, Michael Sangu ‘Mike’ imevunjika huku
mwanaume huyo akitangaza kuoa tena hivi karibuni.
Uhusiano mwingine ambao haukudumu ni wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu achilia mbali Jokate na Alikiba.