Pia Makongojo amepewa adhabu kali,
ikiwemo viboko 12 pamoja na kuamriwa kutoa faini ya Sh milioni 15 mara
atakapomaliza kifungo chake.
Hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya
Wilaya ya Arusha ndani ya chumba cha faragha (chemba) ambako waandishi
hawakuruhusiwa kusikiliza hukumu, lakini baadaye waliambiwa kwa sharti
la hakimu wala waendesha mashtaka kutajwa majina yao kwa sababu kesi
hiyo iliendeshwa faragha.
Awali kesi hiyo ilianza kwa mshitakiwa
kusomewa maelezo yake ya awali akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa Kidato
cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe ambaye hivi sasa
amemaliza masomo.
Awali askari huyo alishushwa pamoja na
mahabusu wenzake mahakamani hapo, lakini kwa kuwa kesi inayomkabili ni
ya ubakaji hivyo inasikilizwa ndani ya chumba cha faragha (chemba)
ambako hakuna ruhusa kwa wanahabari kuandika habari hiyo hadi hapo
hukumu itakapotolewa.
Kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria Namba
186 (3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 ya
Mwenendo wa Makosa ya Kujamiiana ya Mwaka (1998) inayosema kuwa bila
kujali masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusisha makosa ya
kujamiiana, ushahidi au mashahidi watakaohusika hawaruhusiwi kutolewa
kwenye chombo chochote cha habari.
Awali, mshitakiwa huyo kwa mara ya
kwanza alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka lake kwa hakimu
(jina linahifadhiwa) ambako Wakili wa Serikali (jina linahifadhiwa)
alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari
16, mwaka huu katika eneo la Kwa Mrombo, FFU jijini Arusha.
Alidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda
kosa hilo kinyume cha Kifungu cha 130(1 na 2 a) cha Sheria ya Mwenendo
wa Makosa ya Jinai, Sura ya 16.
Baada ya hukumu hiyo kutolewa, mama
mzazi wa mtoto huyo ambaye hakupenda kutaja jina lake, aliiomba serikali
kuingilia kwa makini sheria inayohusu makosa ya ubakaji ili adhabu
itakayotolewa kwa mbakaji iwe kifungo cha maisha badala ya hakimu au
mahakama kutoa kifungo cha miaka 30