|
Na Matukiodaima Blog
WAZIRI wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bw.
Mwigulu Nchemba amejitolea kulipia kiasi cha Tsh milioni 2 kwa
kusaidia matengenezo ya mashine ya maji huku akitumbua majipu kwa
kuwasimamisha kazi viongozi 15 wa bodi ya maji ya kijiji cha Mingela
jimboni kwake Iramba wilaya ya Iramba mkoani Singida baada ya bodi
hiyo kufanya ufisadi wa milioni 9 za mradi wa maji wa kijiji hicho.
Viongozi
hao ambao ni pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mingela, Mwenyekiti,
Katibu, Mhasibu na wajumbe 12 ambao walikuwa wakiunda bodi hiyo ya
maji waliwasimamishwa baada ya kutafuna pesa hizo za mradi wa maji na
kushindwa kulipia milioni 2 kwa ajili ya matengenezo ya mashine
iliyoharibika .
Nchemba
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Iramba alifikia uamuzi huo wa kuivunja
bodi hiyo ya maji kijijini hapo jana baada ya wananchi wa kijiji
hicho kulalamika katika mkutano wake wa hadhara kwa ajili ya
kuwashukuru kwa kumchagua na kuanza kutimiza sehemu ya ahadi zake, kuwa
hawana huduma ya maji safi baada kukosa Tsh milioni 2 za kutengeneza
mashine ya maji iliyoharibika kwa muda sasa.
Kutokana na kilio hicho cha wananchi
Nchemba alilazimika kumwita jukwaani Ofisa Mtendaji wa kijiji
hicho, Bw Said Mussa na bodi yake ili kueleza mapato na matumizi ya
mradi huo wa maji yapo kiasi gani na yapo wapi, swali lililopelekea
viongozi hao kujichanganya kujibu kuwa ni kweli makusanyo ya mradi huo
wa maji ni zaidi ya Tsh milioni 9.4 ila benki zipo kiasi cha Tsh
400,000 na pesa nyingine zimetumika kukarabati mashine hiyo iliyokuwa
ikihitaji kutengenezwa kwa Tsh milioni 2 .
Mganganyiko huu ulimlazimu waziri
huyo kuivunja bodi hiyo ya maji na kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Iramba, Clement Berege kupeleka wakaguzi wa ndani
mara moja katika kijiji hicho ili kukagua mapato na matumizi
pamoja na kuwachukulia hatua wahusika wote wa ufisadi huo wa pesa
za makusanyo ya maji.
Alisema
kuwa ni ufisadi mkubwa ambao umefanywa na viongozi hao wa bodi ya maji
katika kijiji hicho kwa kutafuna pesa zote pasipo matengenezo ya
mashine ya maradi huo wa maji.
“Yaani ni
ufisadi mtupu ambao sikubaliani nao hata kidogo mashine ya
kutengenezwa milioni 2 imetengenezwa kwa milioni 9 na bado haifanyi
kazi …..naomba wote mliohusika na ufisadi huu kuanzia leo mkae
pembeni na wakabidhiwe ofisi watu wengine ……pia mkurugenzi kuanzia
sasa vitabu vyote vya makusanyo ya mapato vithibitiwe ili kuepusha
kupoteza ushahidi ”
Hata
hivyo aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kutuma
wakaguzi wa ndani katika vijiji vyote vya Halmashauri hiyo ili
kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi kwenye vijiji vyote.
Alisema
yawezekana viongozi wa vijiji wamekuwa wakitumia vibaya makusanyo ya
pesa za wananchi bila kufuata utaratibu wa kusoma mapato na matumizi
kwa kila baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa taratibu.
Katika
hatua nyingine, Bw Nchemba aliutaka uongozi wa serikali za vijiji
katika wilaya hiyo ya Iramba kuacha kuendelea kuwatoza wananchi
ushuru kandamizi wa biashara ndogo ndogo hasa zile zilizopigwa
marufuku wakati wa ugonjwa wa kipindupindu kwa kutoza ushuru wa Tsh
10,000 kwa biashara ambayo mwananchi akiuza yote faida yake
anaambulia Tsh 5000 hivyo alishauri uongozi wa Halmashauri kushusha
ushuru huo ambao ulikuwa maalum kwa mapambano ya ugonjwa wa
kipindupindu na kuwatoza ushuru wa Tsh 3500 kwa wananchi
wanaojishughulisha kufanyabiashara ndogo ndogo ikiwemo ya upikaji pombe
kwa ajili ya kuendesha maisha yao.
Pia
alitaka wananchi kuendelea kudumisha usafi katika biashara zao
ili kuondokana na ugonjwa wa kipindupindu, kwa wananchi ambao
walipatwa na maafa wakati wa mvua kubwa zilizonyesha mwaka huu,
alisema kuwa wataalam wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu
watafika kufanya tathimini ili kuwasaidia wananchi hao.
Akijibu tuhuma hizo mbele ya Waziri Nchemba, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mingela, Bw Said Mussa alisema
kuwa ni kweli walikusanya milioni 9.4 za mradi huo wa maji na fundi
kutoka mjini Iramba anahitaji milioni 2 kwa ajili ya kutengeneza mashine
hiyo ila kiasi cha pesa kilichopo benki ni Tsh 400,000 pekee hivyo
hawana uwezo wa kulipia gharama za fundi.
Alisema kuwa kwa upande wake hajui mhusika halisi wa ufisadi huo lakini kwa kuwa waziri amesimamishwa kazi wote basi itasaidia kumpata mhusika
|