Lulu Abassi ‘Lulu Diva.
Stori: Hamida Hassan, Wikienda
Dar es Salaam: Muuza nyago
(video queen) maarufu Bongo, Lulu Abassi ‘Lulu Diva’ ameibuka na kudai
kuwa akikutana na mkali wa Bongo Fleva, Baraka Andrew Odiero ‘Baraka Da
Prince’ hawawezi kusalimiana kwani anamuogopa kama ukoma kwa madai
kwamba alimchonganisha na mpenzi wake, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa
Mitego’.
Akizungumza na Wikienda, Lulu Diva
alisema kuwa Baraka alimpelekea Nay umbeya na kumtangazia ubaya kwa
sababu waliwahi kuingia kwenye uhusiano lakini yeye aliamua kuachana
naye kwa sababu aliona hawatafika mbali.
“Baada ya kuachana na Baraka, alianza
kunitangazia ubaya kwa Nay kuwa sifai, kisa kikiwa ni kumpiga chini
hivyo namuogopa kama ukoma,” alisema Lulu Diva.
Baraka alipotafutwa alimkana Lulu Diva kuwa hajawahi kuwa naye na wala hapendi kumzungumzia.