-Mshindi wa kitita cha milioni 100 kujulikana Jumamosi
Kampuni
ya Murhandziwa Limited ya Afrika ya Kusini ambayo imepewa leseni ya
kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa leo imeanza kuuza tiketi nchini kote na
droo ya kwanza ya mchezo huo itafanyika jumamosi ya wiki ijayo ambayo
mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 100.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa kuuza tiketi jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa
Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania,Abbas Tarimba amesema kuwa
wakati umefika kwa watanzania kushiriki bahati nasibu inayoendeshwa
kitaalamu na inayowezesha washindi kujishindia donge nono na
kubadilisha maisha yao.
“Zawadi
ya milioni 100 sio ndogo itasaidia kubadilisha maisha ya mshindi pia
zitatolewa zawadi mbalimbali na serikali inategemea kupata mapato kwa
njia ya kodi Zaidi ya dola milioni 40 kwa mwaka kutokana na uwekezaji
huu katika sekta hii na aliwataka watanzania wachangamkie kununua tiketi
na kushiriki katika mchezo huu.
Mwenyekiti
wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya Murhandizwa
Limited,Profesa Bongani Aug Khumalo alisema kuwa watanzania wategemee
kuona michezo ya kubahatisha ikiendeshwa kitaalamu na kubadilisha maisha
ya washindi kutokana na zawadi nono watakazopata washindi.
“Tiketi
za Bahati nasibu hii zitauzwa kwa shilingi 500 na zitapatikana kwa
mawakala waliosambaa nchini kote na kwa njia ya mtandao na washitiki wa
mchezo huu wa Bahati Nasibu ya Taifa wanatakiwa kuwa na umri kuanzia
miaka 18 na kuendelea,vilevile droo nyingine za mchezo zitakuwa
zikifanyika kila siku ya Jumatano na Jumamosi na kuwezesha wananchi
wengi kushinda”Alisema.
Alisema
mbali na mchezo huu kuwanufaisha washindi binafsi utawawezesha
watanzania wengi kupata ajira Zaidi ya 1,000 za moja kwa moja na zisijo
za moja kwa moja ambapomkwa sasa imeajiri watanzania 40 na hadi kufikia
mwishoni mwa mwaka huu inatarajia kuwa imeajiri wafanyakazi Zaidi ya
1,000.