Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la
Marekani linaloshughulikia masuala ya kijeshi barani Afrika, Meja
Jenerali Darrly Williams, amemtunuku mkuu wa majeshi ya vikosi vya nchi
kavu Tanzania Meja Jenerali James Mwakibolwa nishani ya ulipuaji bora wa
mizinga nchini.
Nishani hiyo ambayo imekuwa ikitolewa na
Rais wa Marekani, alitunukiwa Meja Jenerali Mwakibolwa baada ya kuwa
mstari wa mbele kurudisha amani kwenye nchi zinazokabiliwa na vita
barani Afrika.
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa
wakuu makamandi wa vikosi vya nchi kavu barani Afrika, uliofanyika
mkoani Arusha, Jenerali Williams alisema jeshi la Marekani barani
Afrika, linamtambua Mwakibolwa kuwa mchapa kazi bora.
“Mwakibolwa ni mtaalamu sana kwenye
masuala ya mizinga, hata tulipokwenda kwenye mafunzo ya kijeshi katika
kambi ya Monduli, tumeona umahiri wake na tuzo hii anastahili kwa kuwa
anafanya vizuri.
“Jeshi la Tanzania limekuwa mstari
wa mbele kutoa kikundi cha M23 kwenye nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) na yote hayo ni kutokana na uchapakazi wa Jenerali
Mwakibolwa,” alisema Jenerali Williams.
Akitoa maoni yake kuhusu tuzo hiyo,
Jenerali Mwakibolwa aliahidi kuhakikisha Jeshi la Tanzania linakuwa
imara zadi barani Afrika.
Alisema Tanzania inazingatia masuala ya kijinsia katika jeshi hilo na sasa asilimia 25 ya wanajeshi ni wanawake.
“Jeshi la Tanzania tuna wanawake
wenye vyeo vikubwa na wako ambao tumewapa kazi kwenye idara mbalimbali.
Tunaamini mwanamke anaweza,” alisema Jenerali Mwakibolwa.
Kuhusu maazimio ya mkutano huo, alisema
wanaangalia namna ya kutoa mafunzo ya kupambana na ugaidi wa baadhi ya
wanajeshi wa Afrika.
Naibu Katibu wa Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la Tanzania, Immaculate Ngwale alisema mkutano huo umekuwa na
faida kwa kuwajengea uimara askari wake