Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania( TCAA)
Mbwana J. Mbwana(wapili kushoto) akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mkuu
wa TCAA, Hamza Johari.(kushoto) wakati
wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, wa kupitia na kujadili
maombi ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa
huduma za usafiri wa anga hapa nchini,uliofanyika leo makao makuu ya
TCAA Banana Ukonga jijini Dar es Salaam. Jumla ya kampuni 27
zimewasilisha maombi ya kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali
nchini ikiwa ni pamoja na Pemba, Dar es Salaam, Mara na Kilimanjaro,Wengine kutokkulia ni wajumbe wa Bodi Hanif M. Malik na Jaffari K. Mpili.
Badhi ya wadau wa usafiri wa anga Tanzania wakiwa kwenye mkutano
wa Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, wa kupitia na kujadili maombi ya
kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa huduma za
usafiri wa anga hapa nchini,uliofanyika leo makao makuu ya TCAA Banana
Ukonga jijini Dar es Salaam. Jumla ya kampuni 27 zimewasilisha maombi ya
kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na
Pemba, Dar es Salaam, Mara na Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akiongea na wadau mbalimbaliwakati
wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, wa kupitia na kujadili
maombi ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa
huduma za usafiri wa anga hapa nchini,uliofanyika leo makao makuu ya
TCAA Banana Ukonga jijini Dar es Salaam. Jumla ya kampuni 27
zimewasilisha maombi ya kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali
nchini ikiwa ni pamoja na Pemba, Dar es Salaam, Mara na Kilimanjaro.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi, Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania(TCAA) Mbwana J. Mbwana(wapili kushto) akiongoza kikao hicho .
Wadau
wa Usafiri wa Anga Tanzania, leo wamekutana kupitia na kujadili maombi
ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa huduma za
usafiri wa anga hapa nchini.
Katika
mkutano huo uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania- TCAA, Banana- Ukonga, jumla kampuni 27 zimewasilisha maombi ya
kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na
Pemba, Dar es Salaam, Mara na Kilimanjaro.Kikao hicho kimeongozwa na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCAA, Bwana Mbwana J. Mbwana na
wajumbe wengine wa bodi hiyo, Prof. Arnold J. Temu, Hanif M. Malik.
Yussuf M. Ali, Jaffari K. Mpili na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza S.
Johari .
TCAA
yenye jukumu la kisheria la kusimamia na kudhibiti masuala ya ki-
usalama, kiuchumi katika sekta ya usafiri wa anga pamoja na kutoa
huduma za uongozaji ndege, hutoa leseni kwa kampuni zinazoomba kutoa
huduma za usafiri wa anga hapa nchini baada ya kampuni hizo kukidhi
vigezo na kanuni zinazosimamia sekta.
Mikutano
hiyo ya kupitia maombi ya leseni za usafiri wa anga hufanyika kila
mwaka ambapo maombi ya kampuni mpya na zile ambazo tayari zinafanya
shughuli zake hupitiwa na wadau na kujadiliwa , kabla ya bodi ya
wakurugenzi wa bodi kuridhia na kutoa leseni kwa kamapuni husika.