Spika wa Bunge Job Ndugai akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mhe Jeanne Uwimanimpaye wakati wa Mkutano huo.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa kwanza kulia) akifurahia jambo na Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega (katikati) na Spika wa
Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi
na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki
uliofanyika Jijini Arusha.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai amemkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa
Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Spika wa Bunge la Afrika
Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda wake.
Spika
Ndugai alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11)
wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika
Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016.
Mkutano
huo pia ulihudhuriwa na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya, Spika wa
Bunge la Kenya, Rais wa Bunge la Seniti la Burundi, Naibu Spika wa Bunge
la Burundi, Naibu Spika wa Bunge la Rwanda, Spika wa Bunge la Afrika
Mashariki pamoja na Makatibu wa Mabunge ya nchi wanachama wa Afrika
Mashariki.
Akiukabidhi
Uenyekiti huo Spika Ndugai aliwashukuru Maspika wenzake kwa ushirikiano
walimuonesha katika kipindi chote cha Uongozi wake na kumtakia kila la
kheri Mwenyekiti mpya wa jukwaa hilo.
Maspika
wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hushika Uenyekiti wa
Jukwaa la Maspika wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo
Tanzania ilichukua Uenyekiti wa Jumuiya hiyo mwaka jana.
Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Kidega atashiki Uenyekiti wa Jukwaa
hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kuukabidhi kwa Spika mwingine
katika mkutano ujao unaotarajiwa kufanyika nchini Kenya.
Pamoja
na mambo mengine mkutano huo wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki ulijadili maswala mbalimbali yanayohusiana
na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Jukwaa la Maspika wa
Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lilianzishwa mwaka 2008.