Mbunge wa Jimbo la Bunda Chadema, Esther.
OFISA Habari wa Chadema, Tumaini Makene leo amesema
mbunge wa Jimbo la Bunda Chadema, Mhe. Esther Bulaya, amekamatwa na
polisi saa saba usiku na kumpeleka kituo cha kati cha jijini Mwanza
akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja
na Wakili John Malya sababu za kukamatwa hazijulikani.Hadi sasa anashikiliwa na polisi. Viongozi wa Chadema wanaelekea kituo cha polisi muda huu kujua hatma yake