
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto)
akimsikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Didas
Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) alipomtembelea ofisini kwake leo
jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo inajishughulisha na udhamini wa
wasanii nchini.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayojishughulisha na uandaaji wa Filamu ya Didas Entertainment
Bibi. Khadija Seif (Dida) (akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni
hiyo wakiwa katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es
Salaam.
Na: Frank Shija
SERIKALI imepongezwa kwa namna inavyotoa ushirikiano na kusaidia wasanii na wadau wa tasnia ya Filamu hapa nchini.
Pongezi
hizo zimetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Didas
Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) alipotembelea ofisi za Bodi ya
Filamu leo jijini Dar es Salaam.
Dida
amesema kuwa kama mdau wa Filamu anaishukuru na kuipongeza Serikali
namna ambavyo inathamini na kutambua mchango wa wadau wa tasnia hiyo
hapa nchini.
“
Naishukuru Serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwetu
sisi wadau wa tasnia ya filamu hapa nchini” Alisema Dida.
Aidha
Dida amesema kuwa kupitia Kampuni yake ya Didas Entertainment yenye
ofisi zake jijini London ipo katika uaandaaji wa Filamu mbili ambazo ni
“Dida” na “Black Belt” zitakazo tengenezewa hapahapa nchini.
Nakuongeza
kuwa filamu hizo zitakuwa shirikishwa baadhi ya wasnii kutoka Nigeria
na zitakapo kamilika Filamu ya Black Belt inatarajiwa kuzinduliwa katika
nchini nne tofauti ambazo ni Uingereza, Nigeria, Ghana na Tanzania
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesma
kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa tasnia Filamu wandani
na njje ya nchi ili kutanua wigo wa tasnia hiyo kukua kwa kasi.
Fissoo ametoa wito kwa wadau wa Filamu kuja kuwekeza katika tasnia Filamu hapa nchini ili kutanua wigo wa filamu za Kitanzania
Didas
Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa tasnia za Filamu na Muziki ambapo
mpaka sasa imewezesha takribani wasanii 30 kupata maonyesho nchini
Uingereza, na imefanikiwa kutengeneza Filamu moja ya “Mateso yangu
Ughaibuni”ambayo inafanya vyema katika soko.Kampuni hii imefungua
milango kwa wasanii wa Filamu ili kutanua wigo wa Filamu za Kitanzania.